.

Monday, August 22, 2011

YAMEMFIKA GADAFFI....................HALI MBAYA TRIPOLI..!!!!!

Mapigano makali yanaendelea katika maeneo yanayozunguka makazi ya kiongozi wa Libya kanali Muammar Gaddafi baada ya majeshi ya waasi kushika udhibiti wa mji huo jana jioni.

Usiku kucha mji huo uligubikwa na sherehe kutoka kwa maelfu ya watu waliokusanyika katikati ya mji huo katika eneo maarufu linatambulika kama uwanja wa kijani(Green Square)
Msemaji wa jeshi la waasi amesema jeshi hilo lilikabiliwa na upinzani kidogo wakati wakilitwaa eneo la mashariki,kusini na magharibu mwa mji wa Tripoli.

No comments:

Post a Comment