.

Thursday, August 11, 2011

WANAWAKE WANAOVUTA SIGARA HATARINI KULIKO WAUME.........


Utafiti mpya umeonyesha kwamba wanawake wenye tabia ya kuvuta sigara wako katika hatari ya kupata maradhi ya moyo zaidi kuliko wanaume wenye tabia hiyo.

Utafiti ulioendeshwa miongoni mwa zaidi ya watu milioni mbili umepata wanawake wako kwenye hatari ya maradhi ya moyo kwa asili mia 25 wakati wanapotumia tumbako.


Sababu za matokeo haya hazijatolowa japo watafiti kutoka Marekani wamesema wanawake wako kwenye hatari kubwa ya kuvuta kemikali zenye simu kutoka kwa sigara ikilinganishwa na wanaume.

No comments:

Post a Comment