.

Sunday, May 15, 2011

ARUKA GHOROFANI NA KUPOTEZA MAISHA.

Bingwa wa Olympiki katika mbio za masafa marefu za Marathon Mkenya Samuel Wanjiru ameaga dunia.
Duru za polisi zinasema, Wanjiru alikumbana na mauti baada ya kuruka kutoka kwa chumba chake cha ghorofa moja katika eneo la Nyahururu, mkoa wa Kati wa Kenya.
Idara ya polisi imethibitisha kifo hicho na kusema kwamba uchunguzi umeanzishwa ili kubainisha sababu za kifo hicho.
Mwanariadha huyo alishinda medali ya dhahabu katika mbio za olimpiki mwaka wa 2008 mjini Beijing, kwa kuweka muda wa 2:06:32. na kuandikisha rekodi ya kuwa mkenya wa kwanza kushinda mbio za marathon kwa upande wa wanaume .
Wanjiru pia alikuwa bingwa wa ulimwengu katika misururu ya mbio za marathon, maarufu kama world marathon majors kuanzia mwaka wa 2008 hadi mwaka wa 2010.
Wanjiru pia aliweka rekodi ya mbio za kilomita 21 kwa kuandikisha muda wa dakika 58:33.
Mwezi Decemba mwaka uliopita wanjiru alifikishwa mahakama, kwa mashtaka ya kutishia kumuua mkewe, kumjeruhi mlinzi wake wa nyumbani na pia kumiliki bunduki aina ya AK-47 bila idhini ya serikali.
Mapema mwaka huu Wanjiru alihusika kwenye ajali mbaya ya barabarani katika barabara ya kutoka Nairobi kuelekea Nyahururu, hatua iliyomfanya kujiondoa kutoka kwa mbio za London Marathon

No comments:

Post a Comment