.

Monday, August 15, 2011

THE GAME AKABILIWA NA MASHTAKA............!!!!!!!!

The Game
Rapa Jayceon Terrell Taylor ''The Game'' anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu baada ya kuweka namba ya mkuu wa kituo cha polisi cha Los Angeles kwenye Twitter na kuwataka mashabiki wake waipige.

Inasemekana aliwaambia wafuasi wake kuipiga namba hiyo ya Kituo cha Campton,California ili awapatie nafasi ya kibarua cha muda cha kujifunza kazi.

Mamia ya mashabiki wa The Game walifuata maelekezo hayo na simu ya kitengo hicho cha polisi ilizidiwa na wingi wa simu zilizopigwa kwa wakati mmoja, na kusababisha kituo kushindwa kutoa huduma za dharura kwa wakati.

No comments:

Post a Comment