.

Tuesday, August 9, 2011

VODACOM MISS TANZANIA YAANZA KAMBI....................

Warembo 30 wanaotarajia kushindana katika mashindano ya Vodacom Miss Tanzania, wakiwa Makao Makuu ya Vodacom, Mlimani City, Dar es Salaam, wakijiandaa kwenda kuanza kambi yao katika Hoteli ya Giraffe.

Warembo 30 kutoka kanda tofauti nchini jana walianza rasmi kambi ya Vodacom Miss Tanzania 2011 kwa ajili ya fainali zilizopangwa kufanyika Septemba 10 kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini.

Malkia wa Vodacom Miss Tanzania 2010, Genevive Mpangala (katikati) akigongeana glasi na warembo hao wanaoanza kambi leo

Mkuu wa Udhamini wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, George Rwehumbiza amesema kuwa sababu kubwa ya kuanzisha utaratibu mpya ni kuwapa nafasi zaidi warembo hao kujifunza mambo mengi wakiwa kambini kama mashindano ya “Big Brother Africa”.

No comments:

Post a Comment