.

Monday, May 2, 2011

BIASHARA YA UTUMWA BADO IPO AFRIKA.

Kampuni moja nchini Uganda, inayojulikana kama Uganda Veterans Development Ltd ilikuwa inatafuta wanawake wa kwenda kufanya kazi katika maduka yaliyo ndani ya kambi za jeshi la Marekani nchini Iraq.
Hakusita na pamoja na wanawake wengine 146 wakatia saini mikataba.
Lakini alipowasili mjini Baghdad, aligundua kuwa kumbe kanunuliwa kama bidhaa na wakala mmoja wa Iraq kwa dola za kimarekani 3,500 sawa na pauni za Uingereza 2,200. Na kazi aliyoajiriwa kufanya ni mhudumu wa ndani kwa familia moja ya Iraq.
Kama wenzake, alilazimishwa kufanya kazi kwa saa nyingi, mara nyingi kuanzia alfajiri saa kumi na moja hadi usiku wa manane. Chakula alichopewa ni kidogo na maji pia ilikuwa shida huku akifungiwa ndani ya nyumba.
Kwa kauli yake, ameiambia BBC kuwa, nilikuwa na kibarua kwa sababu, unavyofahamu Iraq ni nchi yenye mchanga mwingi na hivyo vumbi huongezeka mara kwa mara, kwa hiyo inabidi ufagio usitoke mkononi, alisema Prossie.
Prossie alipojaribu kulalamika kuhusu kazi, aliambiwa na muajiri wake kuwa tumelipa fedha nyingi kukupata wewe na tuliambiwa kuwa nyinyi watu hamchoki wala maradhi hayawezi kuwapata. Kwa hiyo endelea kuchapa kazi.
Prossie alibakwa na mwenyeji wake ndani ya nyumba. Wanawake kadhaa kutoka Uganda waliozungumza na BBC walisema kuwa nao walibakwa pia.
Upande mwingine wa mkoa wa Baghdad, kwenye kituo cha jeshi la Marekani, mlinzi mmoja kutoka Uganda, Samuel Tumwesigye alisikia habari kuhusu yanayowasibu wanawake hawa.
Jitihada zake zikamwezesha kupata simu ya mwanamke anayejulikana kwa jina la Agnes, na kuwasiliana naye akiahidi kusaidia.
Tumwesige anasema kuwa "Jambo la kwanza nililofanya nilikwenda chumbani kwangu nikainama kumuomba Mungu, anisaidie nitekeleze hili nililolianza na nifanikiwe.
Alimuomba Agnes kama angeweza kutoroka kutoka nyumba hiyo na kwenda sehemu moja karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad panapojulikana kama Flying Man statue.

No comments:

Post a Comment