.

Friday, August 19, 2011

WILL SMITH KUREJEA KWENYE RAP.....!!!!!

Will Smith

Nyota wa Hollywood Will Smith anajiandaa kurejea kwenye muziki wa rap kwa kuachia album yake mpya tangu ipite miaka sita akiwa nje ya gemu hiyo ya miondoko ya rap.

Mkali huyo wa filamu ya Men In Black alianza muziki kama The Fresh Prince akiwa na rafiki yake wa utotoni Jeffrey Townes ambapo waliunda kundi la hip hop la DJ Jazzy Jeff & The Fresh Prince.

DJ Jazzy Jeff & The Fresh Prince

Kwa mujibu wa prodyuza  La Mar 'Mars' Edwards, ni kwamba hivi sasa Smith anarejea studio kurekodi ikiwa ni muendelezo wa album ya Lost and Found ya mwaka 2005.

No comments:

Post a Comment