.

Tuesday, August 23, 2011

KIFO CHA AMY WINEHOUSE HAKIHUSIANI NA DAWA ZA KULEVYA....

Marehemu Amy Winehouse

Familia ya mwanadada Amy Winehouse aliyefariki hivi karibuni imesema kuwa vipimo vya kitabibu kupima sumu vimeonyesha kuwa hakukuwa na dawa za kulevya kwenye mwili wake wakati anafariki dunia kama ilivyodhaniwa awali.

Siku ya mazishi ya marehemu Amy

Familia hiyo imesema vipimo vimeonyesha kulikuwa na pombe kidogo sana lakini haijaangaliwa zaidi kama ilichukua nafasi yoyote katika kifo cha mwimbaji huyo aliyefariki dunia mwezi uliopita.

No comments:

Post a Comment