.

Monday, August 1, 2011

AISHA MADINDA ATIKISA EXTRA BONGO......

Nguli wa kudansi nchini Aisha Madinda ameingia kwa kasi ya ajabu katika bendi ya Extra Bongo inayoongozwa na Ally Choki huku akiongeza idadi ya mashabiki na kuifanya bendi hiyo kutoa upinzani wa kutosha kwa bendi nyingine.


Tangu Nguli huyo ajiunge na Bendi ya Extra Bongo akitokea African Stars International ‘Twanga Pepeta’ hivi karibuni, watu wengi wamekuwa wakijitokeza kwenye shoo zinazofanywa na bendi hiyo ambapo muda mfupi tangu ajiunge na bendi yake mpya, idadi ya mashabiki imeongezeka tofauti na siku za nyuma.

Aisha alisema kuwa, kazi hiyo ndiyo msingi wa maisha yake hivyo hatarajii kufanya uzembe kama wengi wanavyofikiri.

No comments:

Post a Comment