.

Wednesday, August 24, 2011

MASHTAKA YA UBAKAJI YA ALIYEKUWA MKUU WA IMF YAFUTWA..........

Dominique Strauss-Kahn

Jaji wa Mahakama mjini New York amefuta kesi ya tuhuma za ngono kwa aliyekuwa mkurugenzi wa Shirika la Fedha Duniani, Dominique Strauss-Kahn.

Hatua hiyo imekuja wakati waendesha mashtaka walitilia shaka uaminifu wa mwanamke anayemshtaki, ambaye ni mhudumu wa hoteli moja, Nafissatou Diallo , mwenye umri wa miaka 32.
Nafissatou Diallo

Bw Strauss-Kahn mwenye umri wa miaka 62, alituhumiwa kumshambulia mwanamke huyo, mhamiaji kutoka Afrika, mwezi wa Mei wakati alipokuwa akiingia chumbani kwake kukisafisha.

Hukumu hiyo inamaanisha kuwa sasa Bw Strauss-Kahn yuko huru, japo bado anakabiliwa na kesi nyingine dhidi ya Bi Diallo.

Dominique Strauss-Kahn na mkewe

No comments:

Post a Comment