.

Wednesday, February 2, 2011

UREMBO

Asilimia kubwa ya watu wazima na vijana wa sasa wamekuwa na muonekano wa weusi kwenye macho pasipo kujua sababu na namna ya kuuondoa.
Huu weusi wakati mwingine unakuwa katika mfumo wa macho kuvimba na husababishwa na vitu vifuatavyo.

Ukosefu wa usingizi, uchovu, msongo wa mawazo, ukosefu au upungufu wa lishe au wakati mwingine dalili ya kuwepo kwa ugonjwa.
Mtu anapokuwa na mafua makali pia macho huonekana meusi na kuwa yamevimba
Kwa watu wenye umri mkubwa mfano kuanzia miaka 40 na kuendelea wanaweza kukumbana na hii hali ikiwa ni ishara ya ngozi kuanza kuzeeka.

Kuepuka hali hii fanya yafuatayo:
 1-Kunywa maji kwa wingi, yani glasi 8 hadi 10 kwa siku kila siku.
 2-Hakikisha unaepuka njia au vitu vinavyofanya uchoshe macho kama vile kutumia kompyuta au kuangalia TV kwa muda mrefu.
3-Hakikisha huachi cream ya aina yoyote katika ngozi ya macho kwa muda mrefu, dakika kumi baada ya kupaka krimu usoni futa kuzunguka macho ili kuiondoa.
4-Unapolala tumia mto ili kunyanyua kiichwa na kuzuia maji maji ya mwili kujilimbikiza katika eneo linalozunguka macho wakati umelala.
TIba:
Weka slesi za viazi kwenye macho ukiwa umeyafunga na uiache kwa dakika 15-20. Au tumia tango la baridi kuweka kwenye macho au majani ya chai (tea bags) iliyokwisha tumika kwa dakika 20.

Paka mchanganyiko wa limao na juisi ya nyanya kwenye sehemu iliyoathirika kila siku mara mbili.

Kila jioni paka mafuta ya mzaituni.

No comments:

Post a Comment