.

Thursday, August 4, 2011

LADY GAGA,TIMBERLAKE WAKALI WA KUTUPIA...........!!!!!


Lady Gaga

Wanamuziki Justin Timberlake na Lady Gaga wameshika nafasi ya kwanza katika chaguo la jarida Vanity 2011 kwa kuwa wasanii namba moja wa kimataifa wanaovaa viwalo vikali kali duniani.Waimbaji hao wamechagulia ikiwa ni sehemu ya mikakati ya jarida hilo ya kumsaka msanii wa kimataifa anaetinga viwalo vikali vya mitindo mbalimbali duniani.


Justine Timberlake


Justine Timberlake akiwa jukwaani
Washindi wengine wanaokubalika kwa kuvaa mavazi mazuri ni pamoja na Johnny Depp, muigizaji Carey Mulligan, Nyota wa "The King's Speech" Colin Firth, mshindi wa Oscar Tilda Swinton pamoja na muigizaji wa "The Social Network's" Armie Hammer.

Johny Depp

OPRAH KUPEWA TUZO YA HESHIMA...........


Opray Winfrey
Malkia wa vipindi vya TV vya mahojiano Oprah Winfrey pamoja na muigizaji James Earl Jones watapatiwa tuzo za heshima katika sherehe za utoaji tuzo za Oscar za mwaka huu.Winfrey ambaye  aliyewahi kutwaa tuzo ya Oscar ya muigizaji bora msaidizi mwaka 1985 kupitia filamu ya ''The Colour Purple'', atapewa tuzo ya Jean Hersholt Humanitarian kutokana na kujitolea kwake mno kutoa misaada.

James Earl Jones
Jones pamoja na msanii Dick Smith watapatiwa tuzo maalum kutokana na kufanya vyema katika kazi zao za uigizaji filamu.

HAPPY BIRTHDAY YOUU...BARACK OBAMA....!!!!!

Rais Barrack Hussein Obama

Leo tarehe 04 Aug 2011 ni siku ya kuzaliwa kwa rais wa 44 wa Marekani Barrack Hussein Obama ambaye anatimiza miaka 50.


Rais Obama akiwa na mkewe Michelle Ohama

Barack Obama alizaliwa mwaka 1961 sawa na taifa la Tanzania ambapo alifunga ndoa na Michelle Robinson October 3,1992 na kufanikiwakupata mtoto wa kwanza Malia Ann mnmo wa July 4,1998 na baadaye Natasha ambaye aliyezaliwa June 10,2001.



Rais Obama na watoto wake Malia na Natasha pamoja na mkewe Michelle katika nyakati za furaha.

Wednesday, August 3, 2011

RIRI ATUPIA KIMALKIA BAJAN CARNIVAL.........!!!!!!








GENEVIEVE KU-ACT MOVIE NA ANGELINA JOLIE..........


Actress wa grade ya juu anayeongozwa kwa kulipwa mkwanja mrefu toka Nigeria,Genevieve Nnaji amepata dili la kuwa starring kwenye movie mpya akiwa na Muigizaji mkali toka Marekani Angelina Jolie Voight mtoto wa Actor John Voight.


kwa sasa Genevieve anahesabika kuwa ni The Biggest African Silver Screen Star kuwahi kutokea Africa na ni the biggest and highest paying role kwenye tasnia ya Movie barani Africa,na pia uvumi uliwahi kutanda kuwa amepata shavu ku-act kwenye movie ya James Bond.

MUONEKANO MPYA WA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHAN...........




MABAIBUI KWA AJILI YA MWEZI HUU MTUKUFU SIO LAZIMA DUKANI HATA MTUMBANI YAPO...!!!!!


Tuesday, August 2, 2011

WAJUE WASHIRIKI WA TPF ALL STARS............!!!!!!MPIGIE KURA UMPENDAE




Patricia Kihoro

Kenya, Age: 25

TPF3: 2009

After leaving the academy, the talented songstress hoped to take her acting and singing to a higher level. She has since collaborated with Harry Kimani in  Stranger Girl and featured in M-Net drama Changes, as Pet. She’s also a news anchor with One FM.



Peter Msechu

Tanzania, Age:23

TPF4- 2010  1st Runners-up

After leaving the academy… He planned to join the university to study music.


Alpha Rwirangira

Rwanda, Age: 25

TPF3- 2009 Winner

After leaving the academy… He expected to succeed in music. He did not work with Gallo Records due to personal reasons. He has obtained a President’s scholarship to study Music and Business at Fulbright University in US.



Caroline Nabulime

Uganda, Age: 27

TPF3: 2009 2nd Runners-up
Caroline Nabulime


Bernard Ng’ang’a

Kenya, Age: 25   TPF3- 2009 1st runner up



Hemedy Suleiman

Tanzania, Age: 25

TPF2: 2008

The musician left the academy hoping to make a name and cause ripples in the Tanzanian showbiz industry.



Amileena Mwenesi

Kenya, Age: 23

TPF4: 2010



Davis Ntare

Uganda, Age: 26

TPF4: 2010 Winner

MWANAMKE MTANZANIA ASHITAKIWA KUMILIKI MTUMWA.............


Mwanake mmoja nchini Uingereza Bi. Rebbeca Balira, mwenye umri wa miaka 47 aishie jijini London ameshtakiwa kwa kosa la kum-miliki msichana wa kazi aitwae Methodia Mathias mwenye umri wa miaka 21 kama mtumwa.

Bi Rebecca Balira ni scientist (HIV expert) anayeaminika kwenye kituo mashuhuri duniani cha utafiti wa magonjwa ya Ukimwi na magonjwa ya kitropical kilichoko jijini London.


Bi Rebecca Balira ameshtakiwa kwenye Mahakama ya mjini London (Southwark Crown Court) kwa makosa mengi yakiwemo;


1. Kum-miliki msichana kinyume cha sheria (kumfanya mtumwa).

 2. Pia bi Rebecca Balira alimnyang'anya passport msichana wake wa kazi na kuificha,

 3. kumfanyisha kazi nyingi bila kumpa muda wa kupumzika (break), kumfanyisha kazi masaa mengi kuanzia alfajiri saa 11 hadi usiku saa 6.

 4. kumfanyisha kazi bila malipo,

 5. kumnasa mabao mashavuni/usoni na kumsina, kumfokea muda wote na mengine mengi.

Kutokana na uchunguzi uliofanywa inasemekana Rebecca Balira alimuahidi mfanyakazi huyo Methodia Mathias kumpatia mshara wa pound £96 za kiingereza (karibia sawa na 250,000 ya Tanzania) kipindi alipokuwa anamchukua nchini Tanzania kumleta Uingereza pesa ambayo ni ndogo sana kwa mfanyakazi wa ndani wa Uingereza kwani ni sawa na pesa ya malipo yake ya siku mbili na sio siku 30. Kwa sheria za Uingereza, unapoajiri msichana wa kazi ni lazima alipwe kiwango kilichopangwa na serikali.

Polisi walipewa taarifa ya kisanga hiki na mtu ambaye alikuwa karibu, mapolisi waliamua kwenda kufatilia walipopewa taarifa na walipofika nyumbani kwa Rebecca na kumhoji alikana kosa na kusingizia kuwa Methodia Mathias ni mtoto wa nduguye. Mapolisi waliamua kumpeleka mahakamani kumfungulia mashitaka kutokana na ushahidi wa mazingira waliyoyakuta mule ndani kwa Rebecca kwani msichana wa kazi hakuwa na chumba chake maalumu cha kulala bali alilala kitanda kimoja na mtoto wa kiume wa Rebecca.

Monday, August 1, 2011

AISHA MADINDA ATIKISA EXTRA BONGO......

Nguli wa kudansi nchini Aisha Madinda ameingia kwa kasi ya ajabu katika bendi ya Extra Bongo inayoongozwa na Ally Choki huku akiongeza idadi ya mashabiki na kuifanya bendi hiyo kutoa upinzani wa kutosha kwa bendi nyingine.


Tangu Nguli huyo ajiunge na Bendi ya Extra Bongo akitokea African Stars International ‘Twanga Pepeta’ hivi karibuni, watu wengi wamekuwa wakijitokeza kwenye shoo zinazofanywa na bendi hiyo ambapo muda mfupi tangu ajiunge na bendi yake mpya, idadi ya mashabiki imeongezeka tofauti na siku za nyuma.

Aisha alisema kuwa, kazi hiyo ndiyo msingi wa maisha yake hivyo hatarajii kufanya uzembe kama wengi wanavyofikiri.