PAUL Merson ameibua zengwe katika klabu ya Arsenal, baada ya kudai kwamba walikuwa wakidungwa sindano za dawa zisizojulikana kila wanapokabiliwa na mechi ngumu.
Nyota huyo wa zamani wa England, Merson, alisema hilo lilikuwa likitokea alipokuwa akikichezea kikosi hicho kinachonolewa na Mfaransa Arsene Wenger.
Katika mahojiano maalumu aliyofanya na jarida la soka la Ufaransa la So Foot, Merson alibainisha kwamba walikuwa wakifanyiwa mambo kama hayo walipokuwa Highbury.
Merson, 43, aliyecheza chini ya Wenger katika msimu wa 1996-97, alisema: “Wakati mwingine, katika mkesha wa mechi kubwa, tunakwenda kambini Holiday Inn huko Islington ambako tunadungwa sindano mikononi zenye dawa tusizozitambua.
“Sijawahi kuuliza swali lolote kuhusu hilo. Kwa kipindi kile tulikuwa tukimwamini kocha, unafanya kila kitu anachotaka wewe ufanye.”
Merson alibainisha kwamba hakujali kitu kwa sababu kwa kipindi hicho yeye binafsi alikuwa chapombe na mtumiaji mzuri wa dawa.
Aliongeza: “Kulingana ilivyokuwa utaratibu wa maisha yangu, ile sikuona ni tatizo kwangu na sikuhofia chochote.”
Merson alibainisha pia kila asubuhi wanapowasili kwenye uwanja wa mazoezi walikuwa wakipewa juisi ya machungwa iliyokuwa imechanganywa na ‘Creatine’.
Creatine inadaiwa kuongeza uwezo wa stamina kwa wachezaji na ndio maana ilikuwa ikitumiwa na Wenger kwa ajili ya wachezaji wake.
Merson, 43, alibainisha kila kitu walichokuwa wakifanya katika kambi ya timu hiyo ya Arsenal akibainisha kwamba wakati mwingine walikuwa wakipewa vidonge vikali vya caffeine kila wanapokwenda kucheza mechi za ligi za ugenini.
Katika kikosi hicho cha Arsenal, Merson alicheza zaidi ya mechi 400 na aliweka wazi hakuijua dawa ya njano iliyokuwa ikitumika kuwadunga kabla ya kushuka dimbani kumenyana kwenye mechi kubwa za Ligi Kuu.
.
Saturday, May 14, 2011
MGANGA AJITOSA KWENYE UMISS.
WAKATI warembo 12 wanatarajiwa kushiriki katika shindano la kumsaka Miss Na Mwandishi
Bagamoyo, kwa upande mwingine limefanikiwa kumuibua mmoja kati ya madaktari wa tiba mbadala ya magonjwa mbalimbali, Dk. Kahenga.
Mashindano hayo ya Vodacom Miss Bagamoyo, yaliyoandaliwa na Asilia Decoration yanatarajiwa kufanyika Mei 28, mwaka huu.
Mratibu wa shindano hilo, Awetu Amir, alisema Dk. Kahenga mwenye sifa kubwa ya utabibu ni mmoja kati ya wadhamini wa shindano hilo.
Mbali na Dk. Kahenga wengine waliodhamini ni Kampuni ya Vodacom na Redds.
Awetu aliwaomba wadhamini wengine kujitokeza kwa wingi ili kufanya mashindano yawe na mvuto.

"NIACHENI NA YANGA YANGU JAMANI"
HATIMAYE mshambuliaji wa FK Jagodina ya Serbia, Mghana Kenneth Asamoah, ametua rasmi jijini Dar es Salaam na kulakiwa na viongozi, wanachama na wapenzi wa Yanga kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Baada ya kutua kwenye uwanja huo, viongozi wa Yanga walikwenda naye moja kwa moja katika Makao Makuu yao yaliyopo katika makutano ya mitaa ya Jangwani na Twiga, jijini, kwa ajili ya kufanya naye mazungumzo ya mwisho ya kuichezea timu hiyo msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara na michuano ya kimataifa.
Mchezaji huyo aliyeteka vichwa vya vyombo vya habari kwa siku za hivi karibuni hapa nchini, aliwasili saa 3:30 asubuhi.
Yanga ilijaribu kumsajili Assamoah kwa ajili ya msimu uliopita, lakini ilishindwa kumtumia kutokana na kukwama kwa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) na hivyo kurejea katika klabu yake ya FC Jagodina, iliyomtoa kwa mkopo.
Na kutokana na kiwango alichokionyesha wakati wa mechi za maandalizi ya msimu uliopita, Yanga wameamua kumfuatilia tena ambapo Mghana huyo ameonyesha nia ya kukipiga Jangwani msimu ujao.
Lakini wakati Yanga wakiendelea na mchakato wao wa kumnasa Assamoah, hivi karibuni, watani wao wa jadi, Simba, walitangaza nia yao ya kuwania saini ya mshambuliaji huyo.
Wekundu wa Msimbazi hao, walifika mbali katika mchakato wao huo, wakidai kuwa jitihada zinazofanywa na Yanga, zitageuka kilio baada ya kufungwa kwa dirisha la usajili wa msimu ujao kwa kuwa watani wao hao wanatumia njia ya mkato.
Mwenyekiti wa Simba, Ismail Rage, aliwaambia waandishi wa habari katikati ya wiki hii kuwa wao wanamfuatilia Assamoah kwa kufuata sheria za Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), kuzungumza na klabu ya mchezaji kwanza badala ya kuanza na mchezaji kama wanavyofanya Yanga.
Rage alisema kuwa kinachofanywa na Yanga kinaweza kuigharimu klabu hiyo iwapo Jagodina watashitaki FIFA na mwisho wa siku, watani wao wa jadi hao, wataishia kunawa.
Kauli hiyo ya Rage ilionekana kuwachanganya wapenzi wa Yanga, wakihisi huenda klabu yao ‘ikaingia mkenge’ kwa Assamoah kama ilivyokuwa msimu uliopita.
Hatimaye jana Assamoah alikata mzizi wa fitina baada ya kutua Jangwani na kusema: “Nimekuja kulipa fadhila Yanga kwa kuwa msimu uliopita klabu hii ilionyesha upendo mkubwa kwangu.”
Alisema Yanga ni timu ambayo anaamini ina umoja na mshikamano, hivyo hiyo ni bahati kwake kuchezea timu hiyo na hayupo tayari kujiunga na timu yoyote nchini hata kwa uhamisho wa fedha nyingi.
Aliwaahidi mashabiki wa timu hiyo kuwa msimu ujao atahakikisha anarudisha ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara inayotarajiwa kuanza Agosti, mwaka huu.
“Ninachoweza kusema kwa sasa ni kwamba nitajitahidi sana uwanjani kama ishara ya kuipenda timu yangu ya Yanga,” alisema Assamoah huku akionekana kuwa na furaha isiyo kifani.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Yanga, Lloyd Nchunga, alisema kuwa ni vigumu timu yoyote kumchukua mchezaji huyo, kwa kile alichodai kuwa bado wana makubaliano na timu anayochezea (Jagodina) kwa sasa.
“Kwa uwezo alionao Kenneth Assamoah, tuna mpango wa kumpa mkataba wa zaidi ya miaka mitatu,” alisema Nchunga.
Kenneth Asamoah, alizaliwa mwaka 1988 katika Mji wa Kumasi, nchini Ghana, ambapo mwaka 2006 alijiunga na Asante Kotoko ya huko na kuichezea kwa miaka miwili kabla ya kujiunga na FK Jagodina inayoshiriki Ligi Kuu ya Serbia ‘Super Liga’.

"MIMI NA SIMBA SC BASI"
OFISA Habari wa Simba, Clifford Ndimbo, ameachia ngazi kutokana na kile alichodai kutopata ushirikiano na uongozi wa klabu hiyo.
Ndimbo jana aliwasilisha barua ya uamuzi wake huo kwa uongozi wa klabu hiyo yenye maskani yake katika Mtaa wa Msimbazi, Dar es Salaam.
Ndimbo bado alikuwa na mkataba na Simba, uliotarajiwa kumalizika Septemba mwaka huu.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Ndimbo alisema kuwa uamuzi huo ni wake binafsi na kwamba hajashawishiwa na mtu yeyote yule.
“Nashukuru kuwa nimefanya kazi nzuri wakati wa uongozi uliopita chini ya Mwenyekiti Hassan Dalali iliyopelekea uongozi wa sasa chini ya Mwenyekiti Ismail Rage kuhitaji kuendelea kupata huduma yangu,” alisema.
Ndimbo alisema: “Kwa kipindi chote ambacho nimekaa na uongozi uliopo madarakani, nimekuwa nikitekeleza majukumu yangu, japo wakati mwingine ni katika ugumu ambao nilipohoji, niliambiwa yote yatatatuliwa.”
Ndimbo alishawahi kuandika barua kama hiyo Aprili 5, mwaka huu na kujadiliwa na Kamati ya Utendaji ya Simba, kabla ya kuzuiliwa na Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Evodius Mtawala.
“Pamoja na uamuzi wake huo wa awali kuzuiliwa na Mtawala, hali ya kutoshirikishwa katika matukio ya klabu hiyo, iliendelea kama kawaida, ikiwamo Machi 28, mwaka huu, ambako katika kikao kilichofanyika Makao Makuu yao, hakushirikishwa na uongozi huo.
“Kudharauliwa na kutoshirikishwa…nimeonekana sina maana ndani ya Simba, hivyo uamuzi huu ni kutoka moyoni na somo kubwa kwangu,” alisema.
Wakati Ndimbo akitangaza kuachia ngazi, Ismail Rage alisema hana taarifa na kwamba yeye si mwajiri wake, bali ni Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Evodius Mtawala.
“Ni cheo kidogo sana cha Ndimbo, hivyo hakiniumizi kichwa na nilipowasiliana na Katibu kuhusiana na taarifa hizi, aliniambia hana taarifa,” alisema Rage.

Tuesday, May 10, 2011
"MATAJIRI MJIANDAE KWA KIBANO.
WAZIRI Kivuli wa Fedha na Uchumi, Zitto Kabwe amesema katika Bajeti ijayo ya Serikali, atapendekeza matajiri wabanwe ili kupunguza makali ya maisha kwa Watanzania walio wengi ambao kwa sasa wanataabika kutokana na umaskini.
"Tofauti ya kipato Tanzania inakuzwa na sababu mbili, moja ni matajiri kuzidi kuwa matajiri na maskini kuendelea kuwa maskini, hivyo hatua za kisera zinapaswa kuchukuliwa kuwazuia maskini kuwa maskini zaidi kwa kuwapunguzia gharama za maisha," alisema Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema).
Alisema katika Bajeti ijayo, atapendekeza kuziba pengo la kodi kwa kupandisha kodi ya kampuni kufikia asilimia 35, kuuza hisa za serikali katika kampuni za Airtel, NBC na BP hivyo kupunguza misamaha ya kodi hadi kufikia asilimia moja ya pato la taifa.
HUU SASA UBAGUZI WA RANGI.
Waziri wa michezo wa Ufaransa amemwondolea lawama kocha wa timu ya taifa ya soka nchini humo Laurent Blanc kuhusiana na ubaguzi wa rangi, baada ya kocha huyo kupendekeza kupunguza idadi ya wachezaji weusi katika timu ya taifa.
Waziri huyo, Chantal Jouanno amesema hakuna ushahidi kwamba Blanc alivunja sheria yoyote kwa kujadili kupunguza idadi ya wachezaji weusi na wale wenye asili ya Afrika Magharibi, wanaojumuishwa katika timu za vijana za Ufaransa.
Blanc amejitetea kwamba alieleweka vibaya.
Kocha huyo pamoja na makocha wengine wa timu za vijana walikuwa wanajadili jinsi ya kuwazuia kwenda kuchezea nchi zingine wachezaji wanaokuzwa nchini Ufaransa.
Bi Jouanno amesema hatma ya mkurugenzi mkuu wa mafunzo katika timu ya taifa Francois Blaquart ambaye alisimamishwa kazi kufuatia kujitokeza kwa habari hizo itaamuliwa na shirikisho la soka la Ufaransa (FFF).
Shirikisho hilo lilitazamiwa kutoa taarifa za uchunguzi wake Jumanne alasiri.
Mapendekezo hayo yamezua tafrani katika shirikisho la soka la Ufaransa, ikiwa bado haijapita mwaka tangu Laurent Blank alipoajiriwa kujenga upya timu ya taifa, baada ya matokeo mabaya kwenye mashindano ya Kombe la Dunia mwaka uliopita nchini Afrika Kusini.
Wavuti wa taarifa za uchunguzi wa kisiri- Mediapart, ulichapisha taarifa kudai Blaquart alipendekeza kupunguzwa kisiri idadi ya wachezaji weusi na wale wenye asili ya Afrika Magharibi hadi kubakia asilimia 30 kwenye baadhi ya vituo vya kutoa mafunzo kwa vijana chipukizi, kikiwemo kituo mashuhuri cha Clairefontaine.
Ilidaiwa Blanc alikubaliana na mpango huo ili kukuza zaidi wachezaji wenye ''utamaduni na histoaria'' ya Wafaransa.
Wakati wa Kombe la dunia wachezaji wapatao tisa katika timu za nchi zingine walikuwa ambao waliwahi kuichezea timu za taifa za vijana nchini Ufaransa.
HIZI NDOTO JAMANI! KILA MTU ATAOTA.
MKAZI wa Mbagala jijini Dar es Salaam, ameibuka na kusema kuwa ameoteshwa na Mungu kutoa dawa kwa njia ya kikombe kutibia wagonjwa wenye maradhi sugu.
Dawa hiyo amedai Mungu amemuotesha kutoa dawa ambayo ni maji ya kisima, bomba na haichanganywi na chochote zaidi ya maji hayo.
Awali kijana huyo aliyekuwa akiabudu dini ya Ukristo na baadae kubadili dini na kuwa Muislam na ndipo ameoteshwa.
Awali imedaiwa kijana huyo alikuwa akifanya kazi ya ukonda katika daladala na hivi karibuni ameibuka na kudai kuwa ameoteshwa.
Kufuatia taarifa hiyo watu wameanza kujitokeza nyumbani kwa kijana huyo kupata kikombe cha dawa hiyo huku akiwa ameshika msaahafu mkononi.
Hata hivyo Kamanda wa Polisi Temeke, wanafanya jitihada za kufanya mahojiano maalum na kijana huyo na taarifa itatolewa kwenye vyombo vya habari.
Kijana huyu ni wa saba kujitokeza na kudai wameoteshwa na Mungu na wengine wamejitokeza katika mkoa wa Mbeya, Moshi, Mbeya, Iringa, Tabora na Morogoro, Pwani wote wakidai kuoteshwa na Mungu kutoa tiba kwa njia ya kikombe.

HUYU NDIYO MTOTO WA KICHINA JAMANI.
Mtoto Lu Hao wa nchini China pamoja na kwamba ana umri wa miaka 3 ana uzito ambao ni mara tano zaidi ya uzito wa mtoto wa umri wake, ana jumla ya kilo 60. Lu Hao, mtoto wa miaka mitatu wa nchini China, alizaliwa akiwa na uzito usiozidi kilo 2.5 lakini hivi sasa ana uzito ambao ni sawa na uzito wa watoto watano wa umri wake wakiwekwa pamoja.
Uzito wa Lu Hao mbali ya kuwashangaza wazazi wake, umewashangaza pia madaktari wa nchini China ambao wameshindwa kujua nini kimemsibu mtoto huyo.
Wazazi wake wamejaribu kila njia ya tiba ya mtoto huyo bila mafanikio na majaribio ya kumlazimisha Lu Hao kula kiasi kidogo cha chakula yamefeli kutokana na mtoto Lu Hao kuangua kilio muda wote mpaka anapopewa chakula chake.
Katika mlo mmoja mtoto huyo huweza kufagia sahani kadhaa za wali na nyama.
"Inatubidi tumuache awe jinsi anavyotaka, tunapomnyima chakula huangua kilio bila kupumzika", alisema mama yake Lu Hao, Chen Yuan.
"Katika mlo mmoja, humaliza sahani tatu kubwa za wali", alisema baba wa mtoto huyo na kuongeza "Tusipompa chakula hufanya vurugu na kuangua kilio siku nzima".
Mtoto Lu Hao anapenda kuogelea lakini hapendi kutembea hali iliyowafanya wazazi wake wawe wanampeleka shule ya chekechea kwa pikipiki.
Wazazi wake wamemtengenezea sehemu ya mazoezi ambapo kila wanapomlazimisha kufanya mazoezi ndivyo anavyosikia njaa zaidi na kula sana na hivyo kuzidi kunenepa.

"JAMANI CONDOM ZIKO WAPI?
Huku Serikali ya Kenya ikiimarisha kampeni dhidi ya UKIMWI, mbinu moja imekuwa kuhamasisha jamii kuhusu kinga kwa kutumia mipira ya kufanyia mapenzi, CONDOM. Kinga hii imefanikiwa katika maeneo ya mijini.
Hata hivyo hali ni tofauti vijijini. Miongoni mwa jamii ya wafugaji, Condom imekuwa ni bidhaa nadra sana kupatikana, hali inayowafanya kutumia njia mbadala, baadhi zikiwa hatari kama alivyogundua Ng'endo Angela alipozuru eneo la Isiolo Mashariki mwa Kenya.
NOELLE AUZA BIKIRA YAKE KWA SHILINGI MILIONI 100.
Mwanafunzi mmoja wa kike wa nchini Ubelgiji mwenye umri wa miaka 21 ameinadi bikira yake na kufanikiwa kupata mteja aliyeinunua kwa takribani Tsh. Milioni 100.
Mwanafunzi huyo aliyejulikana kwa jina moja la Noelle aliunadi mwili wake kwenye mnada wa tovuti ya Yantra ya mjini Amsterdam, Uholanzi ambayo inadili na kuwatafutia wanaume wanawake.
Noelle ambaye ni mwanafunzi anayeishi nchini Ubelgiji, aliamua kuinadi bikira yake nchini Uholanzi huku akificha sura yake ili wazazi wake na marafiki zake wasimgundue.
Baada ya miezi miwili ya mnada huo hatimaye mnada huo umeisha kwa Noelle kufanikiwa kuiuza bikira yake kwa euro 50,000 ambao ni zaidi ya Tsh. Miloni 105.
Noelle atatumia masaa 24 na mwanaume aliyeshinda mnada huo ambaye hajataka kujitambulisha.
Mwanaume huyo mbali ya kupata nafasi ya kuivunja bikira ya kimwana huyo atatakiwa kama sharti la mnada huo ampeleke Noelle kwenye mgahawa wowote ambao Noelle atauchagua.
Noelle anasema kuwa mshindi wa mnada huo atapewa cheti cha daktari kinachothibitisha kuwa Noelle ni bikira. Noelle alisisitiza kuwa tendo la ngono lazima lifanyike kwa kutumia kondomu.
Noelle alidai kuwa aliamua kuinadi bikira yake ili aweze kupata pesa za kujikimu kwenye masomo yake.
Noelle alijinadi kwenye mnada huo kwa kusema kuwa yeye ni mrembo mwenye macho ya hudhurungi, urefu wa mita 1.73, kiuno cha saizi 10 na matiti ya saizi B.
"Mimi ni msichana wa kawaida na wazazi wangu hawatafurahia wakisikia ninainadi bikira yangu", alisema Noelle.
Bei ya kuanzia kuweka dau katika mnada huo ilikuwa ni euro 5,000 (Tsh. Milioni 11).
Katika kuwadhirihishia watu kuwa yeye si kahaba, Noelle alidai kuwa atatoa asilimia tano ya pesa atakazozipata kwa mashirika ya hisani.

ANCELOTTI APATA MKOMBOZI.
Meneja msaidizi wa zamani wa Chelsea Ray Wilkins, amesema meneja wa Chelsea anayekabiliwa na chagizo kubwa la kuondolewa, Carlo Ancelotti hapaswi kutimuliwa mwishoni mwa msimu huu wa ligi.
Lakini Wilkins aliiambia BBC Radio 5: "Sidhani kama klabu inahitaji mabadiliko ya haraka... lakini kwa hakika wachezaji wapya ndio wanahitajika kuongeza nguvu katika kikosi kilichopo.
"Mabadiliko ya jumla, kwa kuanzia kwa kocha, itakuwa ni makosa makubwa."
Chelsea inajiandaa kumaliza msimu bila kombe lolote baada ya kuchapwa na Manchester United siku ya Jumapili, wakiwa na matumaini ya kumaliza nafasi ya pili ya msimamo wa Ligi Kuu ya England.
United pia iliiondoa Chelsea katika mashindano ya ligi kuwania Ubingwa wa Ulaya mwezi wa Aprili.
Meneja wa zamani wa Chelsea Guus Hiddink, aliyeiongoza klabu hiyo kuchukua kombe la FA mwaka 2009, amekuwa akitajwa-tajwa huenda akarejea Stamford Bridge, ingawa kocha huyo Mrusi inaarifiwa hapendelei kazi hiyo.
Waholazi wawili Marco van Basten na Frank Rijkaard pia wametajwa kuwa nao wanaweza wakapewa kazi ya kuinoa Chelsea msimu ujao, pamoja na Andre Villas-Boas, aliyeiwezesha Porto kufika hatua ya fainali ya Europa msimu huu.
Mwengine anayehusishwa kupewa kazi ya kuifundisha Chelsea ni mchezaji wa zamani wa klabu hiyo Gianfranco Zola aliyewahi kuwa meneja wa West Ham.
Ancelotti, ambaye mkataba wake umesalia mwaka mmoja, alikiri siku ya Jumatatu kwamba timu yake haikuwa imara msimu huu, lakini akakanusha mabadiliko makubwa yanahitajika katika kikosi chake.
Monday, May 9, 2011
ALIYEDAI KUBAKWA LIBYA, AFIKA TUNISIA
Eman al-Obeidi, ambaye aliingia ghafla kwenye hoteli moja mjini Tripoli iliyokuwa imejaa waandishi wa habari wa kigeni na kudai kubakwa na wafuasi wa kanali Muammar Gaddafi, amekimbia na kuelekea Tunisia.
Bi Obeidi aliliambia shirika la habari la CNN alivuka mpaka siku ya Alhamis, akisaidiwa na maafisa wa kijeshi walioasi.
Alisema aliondoka Tripoli kwa gari akiwa amefunikwa kichwa huku jicho moja tu likibaki wazi.
Mwezi Machi, aliwaambia waandishi wa habari alishikiliwa kwa siku mbili na kubakwa na askari 15 wanaomtii kiongozi wa Libya.
Tukio hilo lilipata umaarufu mkubwa tangu ghasia kuanza nchini humo, lakini kumekuwa na ripoti nyingine nyingi za ubakaji kama silaha ya vita kulingana na waangalizi.
Picha za kuondolewa kwa nguvu kwa Bi Obeidi kutoka hoteli ya Rixos na maafisa wa usalama wa Libya zilionyeshwa Machi 26 na kushuhudiwa na ulimwengu mzima.
Serikali ya Libya imekana kuwa mwanamke huyo alibakwa, na wanaodaiwa kumshambulia wamefungua kesi kwa madai ya kuwakashifu.
Kulingana na CNN Bi Obeidi ameripotiwa kupelekwa ubalozi wa Ufaransa mjini Tunis mwishoni mwa juma.

"JAMANI SIOI MAPEMA KAMA MNAVYONADHANI".
![]() |
Chris Brown kuptia mtandao Twitter alizima uvumi uliokua umezagaa kuwa alimuomba mpenzi wake waoane wakati wa sikuu za Easter... |
![]() |
CHRIS BROWN AKIWA NA 'DEM WAKE' KARRAUCHE TRAN |
Chis Brown inasemekana kuwa alimuambia dem wake Karrauche Tran kupitia kwenye simu kuwa anamuomba waowane lakini hakuwa na pete kwa wakati huo na mdada huyo kukubali,lakini Chris Brown akafunguka kuwa yeye ni mdogo sana kujihusisha na hizo issue za kuoa kwa sasa coz ndio kwanza ana miaka 21 tu!
MUTHARIKA: NILIOGA MATUSI KUTOKA KWA BALOZI WA UINGEREZA
Rais wa Malawi, Bingu wa Mutharika, ameeleza sababu ya kumfukuza balozi wa Uingereza mwezi uliopita.
Katika taarifa yake ya mwanzo kuhusu ugomvi huo, Rais Mutharika alisema Balozi Fergus Cochrane-Dyet alimtusi, na hayuko tayari kukubali hayo, eti kwa sababu Malawi inapata msaada wake mkubwa kabisa kutoka Ukngereza, kushinda nchi nyengine.
Magazeti yalichapisha barua iliyofichuliwa, ambamo Balozi Cochrane-Dyet alimuelezea Rais Mutharika kuwa anaongoza kimabavu, na hakubali kukosolewa.
Uingereza ilimtaka balozi wa Malawi aondoke London, kujibu kufukuzwa kwa Bwana Cochrane-Dyet kutoka Malawi.

MBABE WA MUAMED ALLY AFARIK DUNIA.
Bingwa wa zamani wa uzito juu mkongwe Sir Henry Cooper, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 76 nyumbani kwa mwanawe Oxted, Surrey.
Katika taarifa yake, Ali alisema amempoteza "rafiki yake wa zamani", akimuita, "mpiganaji hodari na muungwana".
Cooper aliyezaliwa London, aliwahi kushinda tuzo ya Mwanamichezo Bora wa mwaka mara mbili, alitunukiwa cheo cha Sir mwaka 2000.
Pamoja na mabondia wengine hodari wa Uingereza akiwemo Frank Bruno, Tommy Farr na Lennox Lewis, Cooper anaaminika ni bondia hodari Uingereza kuwahi kumpata katika uzito wa juu.
Baada ya kucheza ngumi za ridhaa ikiwemo michezo ya Olympiki ya Helsinki mwaka 1952 akiwa na umri wa miaka18, Henry na pacha wake George, aliyefariki dunia mwaka jana, wote waliamua kujiunga na ngumi za kulipwa wakiwa na umri wa miaka 20 mwaka 1954.
Aliendelea kucheza kwa mafanikio katika ngumi za kulipwa, lakini hakuwahi kushinda taji la dunia hadi alipostaafu akiwa na umri wa miaka 36, mwaka 1971 baada ya kutwangwa na Joe Bugner mwaka mmoja baadae baada ya kutangazwa na BBC kuwa ameshinda Tuzo ya Mwanamichezo Bora wa Mwaka mara mbili, mwaka 1967 na 1970.
Cooper, atakumbukwa sana kutokana na mapambano yake mawili na Ali miaka ya 1960.
Alimuangusha chini kwa konde zito la kushoto lililopewa jina la jina 'Enry's 'Ammer - ukiwa ni umaarufu wa konde lake la kushoto - lakini Ali baadae akashinda pambano hilo lisilokuwa la ubingwa mwaka 1963 katika uwanja wa Wembley.
Ali baadae alizungumza kupitia televisheni ya Uingereza kwamba Cooper "alinipiga ngumi kali hadi wazee wangu Afrika nao wamepata habari".
Akielezea juu ya kifo cha Cooper, Muhammad Ali amesema, "ameishiwa maneno ya kusema" kutokana na kifo cha rafiki yake.
"Henry kila wakati alikuwa na sura ya kutabasamu kwangu; ni tabasamu ya unyeyekevu na upendo", alisema Ali. "Ilikuwa ni jambo jema kuwa karibu na Henry. Nimempoteza rafiki yangu wa zamani. Alikuwa ni bondia hodari na muungwana."
"TUPENI UBINGWA WETU JAMANI"
Manchester United inahitaji pointi moja kutangazwa bingwa wa ligi kuu ya England, baada ya kushinda mchezo wake dhidi ya Chelsea kwa mabao 2-1.
Magoli ya Havier Hernandez katika dakika ya kwanza na bao la kichwa la Nemanja Vidic yaliipa ushindi muhimu kwa Manchester United kusogelea ubingwa.Goli pekee la Chelsea lilifungwa na Frank Lampard.
United walitawala zaidi kipindi cha kwanza, huku Chelsea wakipigana kufa na kupona katika kipindi cha pili.
Man United itakutana na Blackburn Jumamosi ijayo.
BABA HAJI ATOA TALAKA BILA KIFICHO.
Haji Adam au Baba Haji a.k.a "Peoples Choice" wa pili kushoto waliokaa, nguli wa kiwanda cha filamu bongo, tarehe 7/5/2011 ametoa rasmi talaka kwa mzazi mwenziye baada ya kutoelewana kwa kipindi kirefu. Akiongea kwa jazba mzazi mwenziye huyo aliyezaa naye mtoto mmoja na Haji, alilamika kua hapati matunzo mazuri kutoka kwa mumewe huyo kwa kipindi kirefu sasa. Kwa upande wa Baba Haji yeye alisema si kweli maneno ya mzazi mwenziye kwani amekua akimhudumia kama mke halali kabisa wa ndoa kama diani yake inavyoamuru.
Hata hivyo pamoja na kupewa talaka hiyo, mzazi huyo alisema sakata halitaishia hapo kwani atafanya kila mbinu kumchafua mzazi mwenziye huyo kwenye vyombo vya habari ili kumshikisha adabu.
Baba Haji naye akajibu hatojali hata alienda wapi kwani ameshatoa talaka ametoa, anachoangalia sasahivi ni masomo yake.

Saturday, May 7, 2011
"JAMANI MOURINHO JAMANI NDIYO HATUTAMUONA?"
Kocha wa Real Madrid Jose Mourinho amepewa adhabu ya mechi tano kwa mechi za Ulaya, kutokana na matukio wakati wa nusu fainali ya kwanza ya ligi ya mabingwa Ulaya, dhidi ya Barcelona.
Mourinho tayari ametumikia adhabu ya mchezo mmoja kukaa jukwaani, katika mchezo wa pili, na michezo mingine mitano itatekelezwa iwapo atafanya makosa katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.
UEFA pia imemfungia kutocheza mchezo wa fainali kipa wa Barca wa akiba Jose Pinto.
"TOO MUCH IS HARMFULL"
Mbona kila kukicha kuna wimbi la waganga wa jadi wjanajitokeza? hivi hata mikoani kuna mabango ya MGANGA TOKA DAR? Kwanini wasiungane na kujenga hospitali ya pamoja ili tujue kua huduma zao zinapatikana sehemu flani. Mara utaona huyu anatibu hiki mara kile ilimradi tu ni mganga hata kama hana uzoefu na kitu hicho.
Friday, May 6, 2011
Siku kadhaa sasa toka kutangazwa kuuawa kwa kiongozi wa ugaidi Duniani Osama Ben Laden, Jiji la New York City ulinzi umeongezeka maradufu kila pande , hasa sehemu huska ya milipoko ya majengo marefu ya WTC. na ni kituo kukubwa na Train ya chini inayoelekea New Jersey ijulikanayo kwajina la PATH. Sehemu hiyo kama unavyoiona watu wanaendelea kuweka maua kama heshima ya kuwa kumbuka ndugu na jamaa, na vyombo vya habari kutoka kila pande wameweka kambi muda hapo hili mradi tu waweze kutoa habari LIVE kutoka sehemu hii ambayo ujenzi wake unaendelea. Na pia wakimsubiri Mh Rais wa Marekani Barack Obama ambae anakuja siku ya alhamisi kuongea na ndugu na jamaa waliopoteza wapendwa wao. pia kuja kutoa shukrani kwa jeshi lake kwa kazi kubwa waliyoifanya na kufanikiwa kumwangamiza kiongozi huyo wa ugaidi duniani. Picha kwa hisani ya (NY Ebra wa NYC) alietembelea sehemu hiyo kuangalia hali inavyoendelea kwa sasa baada ya kutangazwa kuuawa kwa Osama Ben Laden.
Ulinzi mkali uk5 c X[apey6l0p45-ey o6m-45ks,h -94kiyh7iendelea New York City
Wakaazi wa mji huo wakiendelea kuweka maua Ground Zero
Waandishi wa vyombo mabali mbali vya habari ndani na nje ya Marekani wakiendelea kufunga mitambo yao kwa kuwatangazia wadau LIVE nini kinachoendelea Ground Zero
KOVA: WANAWAKE KUWENI MAKINI.
JESHI la polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limewatahadharisha wanawake nchini, kutodanganyika kuingia katika mahusiano ya kimapenzi na wanaume papo kwa papo kwa kuwa kumekuwa na wimbi la mauaji wanawake baada ya kujitokeza mwanaume anayewarubuni.
Akizungumza na wanahabari Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suileman Kova, amesema amejitokeza mwanaume anayetuhumiwa kuua wanawake waliofikia wanne jijini Dar es Salaam katika maeneo ya Tandika, Keko, Mtoni kwa Azizi Ally na Buguruni kwa Mnyamani katika kipindi cha miezi mitatu.
Amesema mwanaume huyo amekuwa akirubuni wanawake hao kimapenzi kwa kuwaahidi donge nono la fedha na kisha kwenda nao katika nyumba za kulala wageni na kuwalazimisha kufanya mapenzi kinyume na maumbile na anapomaliza haja zake kuwanyonga.
Kova amesema katika uchunguzi uliofanywa na jeshi la polisi limebaini kuwa katika nyumba zote za wageni walizouawa wanawake hao wamebaini ni mwanaume wa aina moja ambaye wahudumu wa nyumba hizo walipoeleza mazingira na maelezo yao yamefafana na kudai kuwa mwanaume huyo hupendelea kuvaa vazi la T-shirt na suruali aina ya jeans, mweupe, mtanashati na kukadiriwa kuwa na miaka 30 hadi 32.
Kova amesema mtuhumiwa huyo ambaye anasakwa ameonekana kuwalenga wanawake ambao wako ndoani [wake za watu] kwa kuwarubuni kuwaahidi fedha nzuri na kasha kuwanyonga na kutokome bila hata kuiba kitu chochote kutoka kwa marehemu.
.
Jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi kumsaka mtuhumiwa huyo kumkamata na kumchukulia hatua zinazostahili na jamii wametakwi kutoa ushirikiano katika suala hilo.

CHACHU NA TAMU YA MAPENZI.
Mwanaume mmoja wa nchini Italia alitumia zaidi ya dola nusu milioni kwaajili ya zawadi na maandalizi ya harusi na mchumba wake lakini siku ya harusi alibaki akilia baada ya kuachwa solemba kanisani huku bi harusi wake akitoroka na mwanaume mwingine.
| Mwanaume wa nchini ya Italia ambaye alionja chachu ya mapenzi baada ya kutorokwa na mpenzi wake siku harusi ameenda mahakamani kudai fidia ya dola za Kimarekani 743,000 kwa kuvunjwa moyo na kuchezewa hisia zake na pia kupoteza kiasi kikubwa cha pesa. Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 32 alitumia pesa nyingi kwaajili ya maandalizi ya harusi na mchumba wake huyo lakini siku ya harusi mchumba wake aliroroka na mwanaume mwingine. Mwanaume aliyetajwa kwa jina moja la Riccardo, alikodisha jumba la kifahari kwaajili ya harusi yao nje kidogo ya jiji la Rome, alikodisha hoteli kwenye kisiwa kimoja cha Pacific kwaajili ya Honeymoon (fungate) na pia aliifanyia marekebisho makubwa nyumba yake ili kukidhi mahitaji ya mke wake mtarajiwa. Kwa mujibu wa shirika la habari la Italia, ANSA, siku ya harusi Riccardo na familia yake na ndugu na jamaa walikuwa tayari kanisani wakimsubiri bi harusi awasili lakini badala yake aliwasili kaka wa bi harusi ambaye alimwambia Riccardo kuwa dada yake hatakuja kwenye harusi. Mchungaji alilazimika kuvunja shughuli zote za harusi baada ya kuambiwa kuwa bi harusi ameteroka na mwanaume mwingine ambaye alikuwa na uhusiano naye wa kimapenzi. Taarifa zimesema kuwa Riccardo amekodisha wanasheria kwaajili ya kumfungulia kesi aliyekuwa bi harusi wake akimtaka yeye na familia yake walipe gharama zote za harusi alizoingia. | ||
"JAMANI MIMI SIYO BILLIONEA NI VIJISENT TU HIVI VYA MBOGA"
MTOTO wa Rais Jakaya Kikwete, Ridhiwani Kikwete ameukana ubilionea aliovishwa na wanasiasa wa vyama vya upinzani.
Amekanusha hayo baada ya Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa na Mwenyekiti wa Chama cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila, kuutangazia umma kuwa ni Ridhiwani Kikwete ni bilionea na kuhoji ubilionea wake umetoka wapi.
Ridhiwani aliwataka Watanzania wasimhukumu kwa kumuona mitaani akiendesha magari ya bei ghali.
“Mi naishi na watu vizuri hapa mjini jamani, tunaishi kimjini mjini na si kila kitu unachomuona nacho mtu ni cha kwake,”, alisema Ridhiwani.
"Hii inatokana na malezi ya wazazi wangu yaliyonieleza kuishi na watu vizuri”, alieleza Ridhiwani
“Hayo wanayonizushia mimi kuwa ni bilionea na namiliki kampuni ya malori 150 na kampuni ya ujenzi pamoja na ghorofa za kupangisha mjini mimi nasema si kweli”.
Alibainisha kuwa habari hizo ni za uongo na uzushi na zimelenga kumchafua yeye na mzazi wake na kupandikiza chuki dhidi ya familia yake na jamii.
Alisema hatua waliyochukua si nzuri na kubainisha kuwa anawaheshimu sana kutokana na umri wao na kuwataka watoe ushahidi wa hayo kwenye vyombo vya habari
Hata hivyo Ridhiwani alibainisha mali zake anazomiliki kuwa ni shamba la hekari moja na nusu lililopo Bagamoyo, gari aina ya Toyota Cami na akaunti mbili katika benki za Stanbic na NBC.

"KWELI BABA YANGU KAUWAWA"
| Mtoto wa kike wa Osama bin Laden amesema kuwa baba yake alikamatwa akiwa hai kabla ya kuuliwa kwa kupigwa risasi mbele yake na wanajeshi wa kikosi maalumu cha Marekani. | ||
| Televisheni ya Al-Arabiya iliwanukuu maafisa usalama wa ngazi za juu wa Pakistan wakisema kuwa binti huyo wa Osama mwenye umri wa miaka 12, aliwaambia kuwa baba yake aliuliwa mbele ya familia yake na kisha mwili wake kuburuzwa hadi kwenye helikopta ya Marekani. Mwili wa mtoto wa kiume wa Osama nao ulichukuliwa na wanajeshi wa Marekani na kupakizwa kwenye helikopta. Televisheni ya Al-Arabiya iliwanukuu maafisa usalama wa Pakistan wakisema kuwa watoto sita wa Osama bin Laden, mmoja wa wake zake na mwanamke mmoja toka Yemen ambaye inasemekana alikuwa daktari wake walisafirishwa hadi kwenye mji wa Rawalpindi karibu na mji wa Islamabad, kupatiwa matibabu kwenye hospitali ya jeshi. "Hivi sasa wanapatiwa matibabu kwenye hospitali ya jeshi ya Rawalpindi" alisema mmoja wa Maafisa usalama wa Pakistan na kuongeza kuwa mke wa Osama bin Laden aliwaambia kuwa wamekuwa wakiishi Abbottabad kwenye nyumba hiyo kwa miezi sita sasa. Afisa mwingine wa ngazi za juu wa Pakistan alisema kuwa baadhi ya taarifa zilizotolewa na Marekani kuhusiana na kukamatwa na kuuliwa kwa Osama hazina ukweli ndani yake. "Hakuna hata risasi moja iliyopigwa toka kwenye nyumba ya Osama, ndege yao ya kivita ilipata matatizo ya kiufundi angani na ilianguka kwenye eneo la tukio". Maafisa usalama wa Pakistan walisema kuwa hawakukuta silaha yoyote wala mabomu wakati walipofanya msako wa nguvu ndani ya nyumba ya Osama baada ya maiti yake kuchukuliwa na Marekani. Uchunguzi wa kwanza ulifanyika jumatatu na jumanne walirudia kufanya msako kwenye nyumba hiyo yenye vyumba 13. Walichokuta ndani ya nyumba ya Osama ni nyati wawili, ng'ombe mmoja na kuku wapatao 150. "Kulikuwa hakuna handaki wala sehemu maalumu ya kujificha ndani ya nyumba hiyo, ndio maana sielewi kwanini mtu anayetafutwa kuliko watu wote duniani alienda kuishi pale", alisema afisa huyo wa Usalama wa Pakistan. | ||
KWELI PALICHIMBIKA.
| Picha hizi za kutisha za maiti za watu waliouliwa ndani ya nyumba ya Osama bin Laden unaweza ukaziona lakini picha za maiti ya Osama bin Laden mwenyewe hautaiona kamwe kwani rais Barack Obama wa Marekani ameishatangaza kuwa picha hizo hazitatolewa kamwe. | ||
| Picha hizi za kutisha zinaonyesha maiti za wapambe wa Osama bin Laden ambao waliuliwa wakati kikosi maalumu cha jeshi la Marekani kilipovamia nyumba ya Osama bin Laden na kumuua Osama bin Laden. Picha hizi zilipigwa na maafisa usalama wa Pakistan ambao waliingia kwenye nyumba ya Osama bin Laden mapema asubuhi ya jumatatu baada ya Marekani kuvamia kwenye nyumba hiyo kumuua Osama bin Laden na kisha kuondoka na maiti yake. Maafisa usalama wa Pakistan ambao hawakutaka kutaja majina yao walizipiga picha hizo na kisha kuziuza kwa gazeti la The Gurdian la Uingereza. Shirika la habari la Reuters limethibitisha kuwa picha hizo ni za kweli na zilipigwa eneo la tukio. Kuhusiana na picha ya maiti ya Osama bin Laden, Rais Barack Obama wa Marekani alisema kuwa picha hizo hazitaonyeshwa kamwe kwani zitasababisha mtafaruku na pia zitatumiwa na wapinzani wa Marekani kueneza propaganda za chuki. Rais Obama alisema kuwa picha za maiti ya Osama bin Laden hazitatolwa na wala picha au video zake wakati akizikwa hazitatolewa lakini aliwahakikishia watu kuwa Osama ameuliwa kweli na kamwe hataonekana tena akitembea kwenye ardhi ya dunia hii. Gonga linki chini kuona picha za hali ilivyokuwa ndani ya nyumba ya Osama bin Laden na picha maiti za watu waliokuwa ndani ya nyumba hiyo. | ||
WANA NDOA SOMENI HII.
| Mwarabu mmoja wa Dubai amefikishwa mahakamani na mkewe na kufunguliwa madai ya fidia ya dola milioni 12.25 kwa kushindwa kumfikisha kileleni mkewe kwenye mambo ya malavi davi na hivyo kumsababishia mkewe mawazo mengi na kumchanganya akili. | ||
| Mke wa mwanaume huyo ambaye hakutajwa jina lake aliiambia mahakama kuwa mume wake alikuwa akizua sababu mbalimbali kumnyima unyumba kwa miezi minne ya mwanzo ya ndoa yao iliyofungwa mwaka 2008. Mwanamke huyo aliendelea kusema kuwa baadae aligundua kuwa mumewe hawezi kazi kitandani kwani alikuwa akisumbuliwa na tatizo la uume wake kutosimama 'dede' hata aimbiwe nyimbo gani, limeripoti gazeti la Gulf News. "Kwa kuangalia misingi ya tamaduni za kiarabu na jinsi mwanamke anavyochukuliwa katika jamii, niliamua kukaa kimya na kujaribu kuizoea hali hii huku nikiomba Mungu mambo yawe sawa", alisema mwanamke huyo. Mwanamke huyo aliiambia mahakama kuwa mumewe ameshindwa kumtimizia mahitaji yake. Aliendelea kuiambia mahakama kuwa mumewe alimsimamisha kazi kabla ya kumuoa na alimvua vidani vyake alivyokuwa navyo wakati huo. Mwanamke huyo anadai fidia ya dirham milioni 45 ambazo ni sawa na dola milioni 12.25 kama fidia ya mumewe kumchanganya akili na kumsababishia mawazo mengi kwa kutomtimizia mahitaji yake. | ||
ALIYEJICHOMA MOTO KUFUNGULIWA MGAHAWA.
MWANAMKE mmoja [32] mkazi wa jijini Dar es Salaam, aliyeweza kujiunguza na maji ya moto ili aweze kuomba barabarani apatiwe mtaji, nduguze wamfungulia mradi wa kuendesha mgahawa eneo la Buguruni.
Chanzo cha habari hii kilidai kuwa, ndugu waliomkataza aachane na kuomba barabarani kwa pamoja walishirikiana kumtafutia mtaji na kumfungulia mgahawa ikiwa ni kumtaka aendeshe maisha yake pasipo kuomba.
Imedaiwa kuwa, mwanamke huyo tayari ameshaanza biashara hiyo mwanzoni mwa wiki hii na kudaiwa kuwashukuru ndugu zake waliojitolea kumfungulia biashara hiyo.
Imedaiwa kuwa, mwanamke huyo anaapa kutokuwa na hamu ya kuolewa kwa kuwa tayari alishapata mateso kutoka kwa mtalaka wake ambaye alimtelekeza na mtoto na kuishi maisha magumu yaliyompelekea kuomba ili ndugu zake waweze kumsaidia.
Imedaiwa kuwa mwanamke huyo alitumia mbinu ya kuomba barabarani ili aweze kupatiwa msada na ndugu zake kwa kuwa ndugu hao hakuna aliyeamini kama angekosa mtaji kwa kuwa ilidaiwa alikuwa na maisha ya juu alipokuwa na mumuwe huyo.

Wednesday, May 4, 2011
KWLI UBISHI NOMA JAMANI.
Mwanaume mmoja toka Urusi ambaye alikuwa akibishana na wageni wake kuwa bingwa wa zamani wa ngumi za uzito wa juu Mike Tyson ni mkali zaidi kuliko wababe wa sasa duniani katika ngumi hizo ndugu wawili wa familia ya Klitscho toka Ukraine, ubishi huo umepelekea mwanaume huyo amuue rafiki yake. Ubishi uliozuka kwenye nyumba ya mwalimu Nikolai Makayev wa mji wa Tyumen nchini Urusi ulipelekea mwalimu huyo awacharange kwa kisu wageni wake wawili.
Katika ubishi huo, Nikolai alikuwa akibishana na wageni wake juu ya nani mkali kati ya Mike Tyson na ndugu wawili toka Ukraine wa familia ya Klitschko ambao hivi sasa ndio wanaotamba duniani katika anga ya ngumi za uzito wa juu.
Nikolai ambaye alikuwa akipata ulabu pamoja na wageni wake hao wawili, alitamba kuwa Tyson ndio mkali zaidi kuliko Vitali Klitschko na ndugu yake Wladimir Klitschko.
Wageni wake walimshutumu Nikolai kuwa hana uzalendo kwa kumshabikia Tyson ambaye ni bondia wa Marekani na kuwaacha akina Klitchko ambao wao ni Warusi.
Nikolai alikasirika kuambiwa hivyo na ghafla alichukua kisu na kuanza kumshambulia mgongoni mmoja wa wageni wake.
Mgeni mwingine ambaye naye alikuwa ni rafiki wa karibu wa Nikolai, aliamua kukimbilia nyumbani kwake kunusuru maisha yake ingawa naye alikuwa tayari ameishajeruhiwa kwa kuchomwa na kisu na Nikolai.
Polisi waliitwa lakini hadi wanafika tayari Nikolai alikuwa ameishamuua mmoja wa wageni wake.
Vifo vinavyosababishwa na pombe vimekuwa vikiongezeka nchini Urusi ambapo watu 500,000 huuliwa au hufariki kutokana na ulevi.
Hali hiyo imewaathiri zaidi wanaume nchini Urusi ambapo wanaume wengi wamekuwa wakifariki kutokana na ulevi au matatizo yanayotokana na pombe, hali hiyo imesababisha kuwe na idadi kubwa ya wanawake kuliko idadi ya wanaume nchini Urusi.

"KUMBE OSAMA HAKUA NA SILAHA NYUMBANI KWAKE?"
Kiongozi wa kundi Al-Qaeda Osama Bin Laden hakuwa amejihami wakati alipouawa na majeshi ya Marekani siku ya jumapili baada ya kukataa kukamatwa, ikulu ya White House imesema.
Shirika la kijasusi la Marekani(CIA) limesema halikujulisha Pakistan kuhusu uvamizi huo kutokana na hofu kuwa huenda ingehatarisha operesheni yao.
Pakistan imekanusha ufahamu wa uvamizi huo na idara ya ujasusi wa nchi hiyo imesema imeaibika na kutofaulu kwao.
Maafisa wa Marekani wamesema bado hawajaamua lini watoe picha ''za kutisha'' za mwili wa Bin Laden.
Lakini mkurugenzi wa CIA Leon Panetta ameiambia kituo cha televisheni cha NBC nchini Marekani kuwa bila shaka picha ya mwili wake itatolewa wakati mmoja.
Msemaji wa ikulu ya White House Jay Carney amesema mke wa Bin Laden alipigwa risasi kwenye mguu wake lakini hakuuawa.
Jumapili iliyopita, ikulu ya White House ilisema mwanamke huyo aliuawa katika makabiliano baada ya Bin Laden kumtumia kama ngao.
Bin Laden, mwenye umri wa 54, alikuwa mwanzilishi na kiongozi wa kundi la al-Qaeda. Inaaminika aliamuru mashambulizi yaliyotokea mjini New York na Washington 11 Septemba 2001, pamoja na mashambulizi mengine ambapo watu waliuwawa.
Subscribe to:
Posts (Atom)