.

Friday, August 19, 2011

SALMA DACOTHA LIVEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE

                                             Mwami hapa km anasema tatu bila
                                   Jamani jamani simba walijua kunipa raha,kumbe afande hapo nyuma nae simba.
 
Nimepiga jezi yangu kwa raha zangu,afande kasahau hadi kazi yake
       ha ha ha ha haaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

 
TCHAOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO

LILIAN WA BLU3 AACHIA VIDEO MPYA........!!!!!

Lillian Mbabazi
Nyota wa kundi la Blu3 Lillian Mbabazi wa Uganda ameibuka na video yake mpya aliyoipa jina la 'Kankutwale' ambapo ameweza kumpa shavu msanii Diamond Oscar kutoka kundi la Goodlyfe pamoja na washkaji zake wa karibu wa kike wa Lillian.

Diamond Oscar

JIM IYKE NA KATE HENSHAW NUTTAL WATEMWA DILI LA NOTI..........

Jim Iyke
Kate Henshaw Nuttal

Wakali wa filamu kutoka Nigeria Jim Iyke na Kate Henshaw Nuttal wametemwa katika dili la fedha za nchi hiyo la mamilioni ya naira la kuwa balozi wa Globacom ambapo mkataba wao na kampuni hiyo umefikia kikomo na wameafikiana kutoendelea nao tena.

Kunle Afolayan

Wakati huo huo nyota wa Nollywood pamoja na maprodyuza Odunlade Adekola na Kunle Afolayan wameteuliwa rasmi kuwa mabalozi wapya wa Glo na watalipwa naira milioni 10 kwa mwaka.

Odunlade Adekola

WILL SMITH KUREJEA KWENYE RAP.....!!!!!

Will Smith

Nyota wa Hollywood Will Smith anajiandaa kurejea kwenye muziki wa rap kwa kuachia album yake mpya tangu ipite miaka sita akiwa nje ya gemu hiyo ya miondoko ya rap.

Mkali huyo wa filamu ya Men In Black alianza muziki kama The Fresh Prince akiwa na rafiki yake wa utotoni Jeffrey Townes ambapo waliunda kundi la hip hop la DJ Jazzy Jeff & The Fresh Prince.

DJ Jazzy Jeff & The Fresh Prince

Kwa mujibu wa prodyuza  La Mar 'Mars' Edwards, ni kwamba hivi sasa Smith anarejea studio kurekodi ikiwa ni muendelezo wa album ya Lost and Found ya mwaka 2005.

Thursday, August 18, 2011

KAA TAYARI KWA DEVIL'S KINGDOM............!!!!!!!


Filamu ya Devil's Kingdom ya nguli wa filamu nchini Steven Kanumba ambayo inakadiriwa kutumia mamilioni ya fedha katika utengenezaji wake na ikiwashirikisha nyota wakali wa filamu wa hapa nyumbani na pia kuwa filamu pekee iliyoweza kumleta msanii kutoka nje ya nchi inatarajiwa kutoka hivi karibuni kaa tayari.

Baadhi ya washiriki wa filamu hiyo wakati wa upigaji picha

Gwiji huyo ametumia fedha hizo ikiwa ni pamoja na ujio wa Super Star Ramsey Noah kutoka nchini Nigeria kwa ajili ya kuja kurekodi filamu hiyo ya aina yake na kuweka historia kwa kampuni yake kuonyesha nia zaidi ya kuipeleka mbele sanaa hiyo ya filamu kwa kuwashirikisha nyota wakali kutoka sehemu mbalimbali kwa ajili ya kuwakutanisha na wasanii wa hapa nyumbani kupitia kazi zao na kupata uzoefu kutoka kwa wasanii hao.
Ramsey Noah na Steven Kanumba

FAST AND FURIOS 6 KUTOKA 2013.........!!!!!!


Vin Diesel

Movie kali inayotikisa ya series ya mwigizaji wa filamu za kibabe, Vin Diesel inayokwenda kwa jina la Fast and Furious 6 imepangwa kuachiwa mwaka 2013.

Filamu iliyotokisa ya Fast 5

Filamu hiyo inayohusu uhalifu wa genge moja la kutengeneza fedha imetengenezwa chini ya mtayarishaji maarufu Justin Lin inatarajiwa kuwa tishio zaidi ya zile zile zilizopita.

Mtayarishaji wa Fast and Furios Justin Lin

Movie ya mwisho kutoka ya hivi karibuni ya Fast Five imeonyesha mafanikio kwa kuuza jumla ya nakala dola milioni 600 duniani kote.

Baadhi ya utamu wa vipande vya movie ya Fast Five.........




''BEYONCE KAMA MICHAEL JACKSON''............!!!!!!

Beyonce akiwa on stage

Rapa Shawn Carter''Jay Z'' amemwagia sifa mkewe mwanadada Beyonce Knowles kuwa anamuona kama Michael Jackson wa pilia liyebaki duniani.

Beyonce na Jay Z

Jay Z amesema katika chombo kimoja cha habari nchini Marekani kuwa ufanyakazi kazi wa nguvu wa mke wake ndio unaoumpa shoo nyingi na kuwafanya baadhi ya watu kufikiria kuwa anafanya kazi kwa mashine ambapo amesema uwezo huo ameuona wakati anamsindikiza kufanya onyesho la kutangaza albamu yake ya nne.

Mfalme wa Pop Michael Jackson enzi za uhai wake akifanya shoo

Jay Z anasema anamuona mkew kama Michel Jackson wa pili aliyebaki duniani baada ya kwanza kufariki akiwa na miaka 50.

YANGA ILIVYOLIWA 'DAKU' NA SIMBA............!!!!BAO 2-0......

Kibao kikionyesha 2 bila Live!!!!!

Mabao mawili kutoka kwa wachezaji Haruna Moshi ‘Boban’ na Felix Sunzu yalitosha kuinyamazishaa Yanga katika mchezo wa Ngao ya Jamii uliopigwa jana usiku katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kufanya Simba iibuke na ushindi wa mabao 2-0.

Timu ya soka ya Simba kabla ya mechi kuanza
Simba na Yanga zikimenyana katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam
Mchezaji wa Simba Uhuru Selemani akinyanyua juu ngao ya hisani mara baada ya kukabidhiwa rasmi katika mchezo huo.
Mashabiki wa Simba wakishangilia Game jana ilikuwa raha tupu
Wachezaji wa Simba wakishangilia kutoka kulia ni Emmanuel Okwi, Victor Costa, Uhuru Selemani, Felix Sunzu na Juma K. Juma.

ASKARI WAFANYA NGONO KITUONI.............!!!!

Jeshi la Afrika Kusini limeingia kwenye kashfa baada ya Askari wawili toka nchini humo kujulikana kuwa walifanya mapenzi wakiwa kazini tena na uniform za kazi.
Shuka chini ushuhudie tukio by tukio........

Kwa hisani ya www.chiniyacarpet.blogspot.com....unaweza kutembea kila siku kwa habari za burudani ambazo hazijachakachuliwa mahali popote.....

Wednesday, August 17, 2011

ELIZABETH AJIFUNGUA BABY MALAIKA...........!!!!!!!

Baby Malaika

Wanandoa Elizabeth Gupta na Kelvin ambao walikuwa washiriki wa shindano la Big brother mwaka 2009 wamebahatika kupata mtoto wa kike waliyempa jina la Malaika....Blog hii inawatakia kila la kheri katika malezi ya mtoto wao huyo......


Wazazi wapya Kelvin na Elizabeth

LIL WAYNE NA DRAKE KUPIGA COLLABO......

Lil Wayne

Rapa Lil Wayne na Drake wanafuata nyayo za Jay-Z na Kanye West kwa wao nao pia kuungana pamoja ambapo mkali huyo wa kibao cha Lollipop amekuwa na mchango mkubwa katika mafanikio ya Drake kama msanii solo na sasa anashinikiza kuwepo kwa mipango ya kufanya kazi pamoja.

Drake

Bosi wa lebo anayoifanyia kazi Wayne ya Cash Money Records Bryan Birdman Williams amenukuliwa akisema yeye na Wayne wamekuwa wakizungumzia juu ya project ya pamoja baina ya Wayne na Drake.

Tuesday, August 16, 2011

MBUNGE ATOLEWA NJE KWA KUVAA HERENI..........

Sonko akiwa katupia hereni bungeni

Mbunge machachari wa bunge la Kenya Mbuvi Sonko jana alitolewa bungeni kwa mara ya pili kutokana na kuvaa hereni zenye kung'aa bungeni kama wafanyavyo mastaa na vijana wa kisasa.

Mbunge wa Jimbo la Ikolomoni Bonny Khalwale alikuwa wa kwanza kuhoji jinsi Mbuvi alivyovaa bungeni baada ya kuiona hereni sikioni mwake, hata hivyo spika Kenneth Marende akawa hajashtukia issue.

Lakini mbunge wa Kisumu Magharibi Olago Aluoch alisimama naye kuhoji Mbuvi alivyovaa bungeni na safari hii Spika Marende akamuamuru atoke nje kwa siku nzima hapo ya jana, licha ya kukanusha na kuwataka wabunge wenzie wamkague kama ameificha hereni.


Sonko katika swaga zage

Monday, August 15, 2011

THE GAME AKABILIWA NA MASHTAKA............!!!!!!!!

The Game
Rapa Jayceon Terrell Taylor ''The Game'' anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu baada ya kuweka namba ya mkuu wa kituo cha polisi cha Los Angeles kwenye Twitter na kuwataka mashabiki wake waipige.

Inasemekana aliwaambia wafuasi wake kuipiga namba hiyo ya Kituo cha Campton,California ili awapatie nafasi ya kibarua cha muda cha kujifunza kazi.

Mamia ya mashabiki wa The Game walifuata maelekezo hayo na simu ya kitengo hicho cha polisi ilizidiwa na wingi wa simu zilizopigwa kwa wakati mmoja, na kusababisha kituo kushindwa kutoa huduma za dharura kwa wakati.

JESSICA ALBA AJIFUNGUA MTOTO MWINGINE..........!!!!!!

Jessica akiwa na mumewe Cash Warren

Muigizaji nyota Jessica Alba amebahatika kupata mtoto mwingine wa kike ambapo amejifungua siku ya Jumamosi ya tarehe 13 na kumleta duniani ndugu wa mtoto wake wa kike mwenye miaka 3.

Jessica na mtoto wao mdogo

Alba ambaye ni nyota wa Sin City alitangaza kupitia mtandao wa facebook kuwa yeye na mume wake Cash Warren wamepata mtoto mwingine na wana furaha sana.

Jessica na mumewe pamoja na mtoto wao mkubwa wa kike

TUSKER PROJECT ALL STARS YAMALIZIKA........!!!!!MSECHU ASHINDA........


Peter Msechu wa Tanzania

Shindano la Tusker All Stars lililoanza 26 June,2011 limefikia fainali jana kwa washindi watatu kupatikana ambapo Alpha Rwirangira toka Rwanda (TPF 3 - Winner),Peter Msechu toka Tanzania (Mshindi wa 2 – TPF 4) na Davis Ntare toka Uganda (TPF 4 – Winner) wameibuka washindi na wamepata shavu la kupiga show same stage na wasanii wa kimataifa baadaye mwaka huu nchini Kenya.

Alpha Rwirangira toka Rwanda (TPF 3 - Winner)

Washiriki wengine walikua Hemedi Suleiman toka Tanzania,Caroline Nabulime na Amileena Mwenesi toka Kenya,Bernard Ng'ang'a na Patricia Kihoro toka Kenya walishiriki na walikaa wiki 8.

Davis Ntare toka Uganda (TPF 4 – Winner)

CHAMELEONE ABADILI DINI.........!!!!!


Chameleone akiwa anapongezwa

Mwanamuziki nguli nchini uganda Jose Chameleone ameamua kubadilisha dini na kuwa muislamu ambapo alisilimu kwenye msikiti wa Kibuli jijini Kampala na amedilisha jina la Joseph na kujiita Gadaffi.

Akiwa katika matukio tofauti ndani ya msikiti wa Kabul