.

Friday, July 22, 2011

MODEL WA JLO NDANI YA SCANDAL YA NGONO.............


William Levy model kutoka nchini Cuban ambaye alihusishwa kimahaba na mwanamuziki Jennifer Lopez baada ya kutangaza kuachana na mumewe hivi sasa yupo katikati ya skendo ya ngono.


Mwigizaji uyo nyota maarufu kama Juan Miguel ambaye alicheza kama mpenzi wa Jlo katika video ya ''Into You video'' hivi sasa anapamba vichwa vya habari kwa kukabiliwa na tuhuma za kujihusisha na mahusiano na binti wa miaka 17 mwaka jana ambapo binti huyo ametoa tuhuma kuwa Levy alimlazimisha kufanya naye ngono katika chumba cha hoteli na anadai dola milioni 2.5 kwa uharibu aliofanyiwa.

RIHANNA ASIKITISHWA NA KIFO CHA FAN WAKE...........


Mwanamuziki Rihanna ameguswa na kifo cha shabiki wake kijana aliyefariki kwa ajali ya gari huku akisikiliza nyimbo zake ambapo mkali huyo wa kibao Umbrella alichanganyikiwa baada ya kubaini shabiki yake huyo Karen mwenye miaka 17, anaye miliki kurasa maalum ya twitter kwa ajili ya Rihanna amefariki katika ajali.


                                      
                                           
Rafiki wa kijana huyo alimuhabarisha Rihanna kuhusiana na tukio hilo kupitia  kwenye tuvuti ya jamii na ndipo Rihanna alipoandika ujumbe wa rambirambi uliosema shabiki wangu mkubwa amefariki dunia hii leo akiwa na umri mdogo, Karen umetutoka hatutakusahau daima.

R.KELLY APATA NAFUU



Nyota wa muziki wa soul R. Kelly ameanza kupata nafuu huko Chicago, katika hospitali Illinois baada ya kufanyiwa upasuaji wa dharura kwenye koo lake.


Mwimbaji huyo wa kibao cha I Believe I Can Fly alikuwa na tatizo katika mfumo wa koo kuanzia jumanne ya wiki hii ambapo msemaji wake Allan Mayer amebainisha kuwa R. Kelly ataendelea kulazwa katika hospitali hiyo ya Kaskazini Mashariki mwa Chicago kwa muda usiojulikana.

KATTY PERRY AONGOZA TUZO ZA MTV BASE...................


Nyota wa muziki wa Pop nchini Marekani Katy Perry anaongoza katika tuzo za mwaka huu za MTV base kwa kuteuliwa kuwania tuzo hizo katika vipengele tisa ambapo baadhi ya tuzo anazowania ni pamoja na video bora ya mwaka, video bora ya Pop pamoja na video yenye best special effects.


 
Mwanumuziki kutoka nchini Uingereza Adele pamoja na Kanye West wameteuliwa kuwania tuzo kwenye vipengele saba ambapo wasanii wengine walioteuliwa zaidi ya mara moja ni Lady Gaga, Beyonce pamoja na Bruno Mars.




Katty Perry anatamba na ngoma kali kama "California Gurls" na "Teenage Dream"anaweza kunyakua tuzo kibao katika vipengelea alivyochaguliwa.

Thursday, July 21, 2011

CHRIS BROWN APATA DILI LA MOVIE........


Nyota wa R&B kutoka nchini Marekani Chris Brown anatarajiwa kuonekana katika filamu mpya ya vichekesho itakayotokana na story iliyoandikwa na Steve Harvey kwenye kitabu chake cha Ac Like a lady,Think like man ambacho kilikuwa kitabu chenye mauzo ya hali ya juu.


Filamu hiyo inatarajiwa kuwa na jina la ''Think Like a man'' ambayo pia itawashirikisha waigizaji kama Kevin Hart,Michael Ealy,Gabrielle Union,Regina Hall,Lala Vasques na 'Entourage' Jerry Ferrara.

RIHANNA AKIKATA MITAA NA KIVAZI CHAKE.................


Mwimbaji wa R&B Rihanna amejikuta akiwaacha wakazi wa New Jersey Marekani mshanga kutokana na kuvaa kivazi cha mitego na kutembea nacho mtaani.


Nyota huyo anayetamba na kibao cha S&M  alionekana akikata mitaa bila wasiwasi wakati wengine walidai alikuwa anatafuta chumba cha kulala lakini hakuweza kulala hapo na badae kurejea jijini New York.

Wednesday, July 20, 2011

AWAUA WAZAZI WAKE NA KUANGUSHA PARTY NYUMBANI



Kijana mmoja wa kiume katika jimbo la Florida nchini Marekani anatuhumiwa kuwauwa wazazi wake kwa kuwapiga nyundo na kisha akafanya tafrija yaani party amefikishwa mahakamani.

Kijana huyo ambaye ametambuliwa kwa jina la Tyler Hadley, mwenye umri wa miaka 17 anatuhumiwa kuwauwa wazazi wake Blake na Mary-Jo Hadley siku ya jumamosi na kisha akawafuingia miili hiyo chumbani na kuwaalika wageni  katika hafla hiyo.

Amefunguliwa mashitaka kama mtu mzima lakini hatahukumiwa kifungo cha kifo kwa kuwa umri wake ni mdogo na chanzo cha mauaji hayo bado hakijajulikana.

''MAMA G'' KUNG'ARA KATIKA FILAMU MPYA.......


Mwigizaji nyota wa filamu nchini Nigeria Patience Ozokwor maarufu kama '''Mama G'' anatarajiwa kushiriki katika filamu mpya nchini Malawi iitwayo ''The Return''.

Katika filamu hiyo Mama G kama kawaida yake ataigiza kama mama mwenye roho mbaya anayewatesa watoto yatima na kuwatumikisha kazi watoto hao kwa ajili ya kujiongezea kipato.


Mama G pia anatarajiwa kufanya ziara kwa kutumbuiza live stejini katika miji mitatu ikiwemo Lilongwe,Blantyre na Mzuzu.

TREY SONGZ NDANI YA MOVIE KALI............


Nyota mkali Trey Songs amesaini mkataba wa ku-act kama starring kwenye remake ya movie ya kutisha iitwayo ''Texas Chainsaw Massacre'' itakayokua katika mfumo wa 3D....


Texas Chainsaw Massacre ilitengenezwa mwaka 1974 chini ya Directer John Lussenhop (aliyengeneza pia movie kali ya movie Takers,na Trey Songz humo ndani ame-act kama boyfee wa mdada Alexandra Daddario Movie hiyo inatarajiwa kuanza kutengenezwa mwezi huu pande za Shreveport, Lousiana na inatarajiwa kuwa kwenye theaters mwakani mwezi October,2012

SWIZZ BEATZ KUMSAIDIA RAFIKI YAKE DMX


Produza mkali Swizz Beatz ameamua kumfikia rafiki yake DMX kwa kumpa ofa ya kumsaidia rapa huyo aliye matatani kurejea tena katika gemu baada ya kuachiwa huru kutoka gerezani siku ya Jumanne.



DMX ambaye jina lake halisi ni Earl Simmons aliachiwa jela kutoka gereza la Arizona baada ya kutumikia kifungo cha miezi saba, kutokana na kukiuka masharti ya kuwa chini ya uangalizi, lakini sasa anataka kurejea studio baada ya kukutana na familia yake.

Nyota wa hip hop Swizz Beatz ambaye ni mshirika wa karibu wa DMX, pia ni memba wa kundi la Ruff Ryders amesisitiza kuwa anamgojea DMX kumpigia simu ili warejee tena mzigoni.

MODEL AKANUSHA KUTOKA NA JLO...........



Model ambaye ameshiriki katika video mpya ya Jennifer Lopez amekanusha uvumi kuwa ana mahusiano ya kimapenzi na mwanamuziki huyo ikiwa ni siku chache tu kupita tangu atengane na mumewe.


Model huyo aliyetamba katika tamthilia ya ''don't mess with an anjel'' huyo William Levy maarufu kama Juan Miguel au Brad Pitt wa Cuba anaonekana katika video hiyo akiwa kimahaba ufukweni na J-LO huku akimbambia katika video ya wimbo wa I'm Into You.


Levy alitengana na mkewe Elizabeth Gutierrez mwezi mmoja baada ya kushutiwa video hiyo Aprili mwaka huu ambapo J-Lo naye ametangaza kutengana na mumewe Marc Anthony Ijumaa ya wiki iliyopita.

Tuesday, July 19, 2011

NJAA SOMALIA INAZIDI KUTISHIA............


Hali ya njaa katika nchi ya Somalia inazidi kuwa mbaya na Umoja wa mataifa umelenga kutangaza kuwa sehemu kadhaa nchini humo zinakabaliwa na janga la kimataifa kufuatia hali hiyo.


Maelfu ya familia yapo katika hali mbaya ya uhitaji wa chakula na maji na wanatembea mwendo mrefu kutoka nchini Somalia mpaka katika makambi ya wakimbizi ya Dadaab huko  mashariki mwa Kenya.






Hali ya ukame iliyolikumba eneo hilo haijawahi kuonekana kwa zaidi ya miaka 60 na umoja wa mataifa umeielezea hali hiyo kuwa ni eneo la dharura kwa binadamu.

Wakati huo huo Umoja wa Mataifa umesema kuwa mashirika ya kutoa misaada yanahitaji kupata hakikisho zaidi kutoka makundi ya wapiganaji kabla kupeleka misaada nchini humo.

AISHA MADINDA HUYOOO KWA CHOKI.....



Aliyekuwa mnenguaji mahiri wa bendi ya African Stars wana wa kutwanga na kupepeta Aisha Madinda amehamia rasmi bendi ya Extra Bongo kwa Mzee wa farasi Ally Choki na kuungana na mwalimu wa madansa Super Nyamwela kusongesha mzigo katika bendi hiyo inayokuja kwa kasi ya ajabu katika muziki wa Dansi Tanzania.





Kuna habari kuwa aliyekuwa mshindi wa kimwana manywele wa twanga pepeta kwa mwaka 2011 amechukua nafasi yake kwenye bendi hiyo kutokana na umahiri wake wa kudance.

HONGERA DIDA WA ''G''...........!!!!!!!!!!!!


Mtangazaji maarufu wa kipindi cha ‘Mitikisiko ya Pwani’ cha kituo cha radio cha Times FM Khadija Shaib ‘Dida wa G’ amefunga ndoa tena na mwanamume wake kipenzi aitwaye Gervas Mbwiga ambapo sherehe hizo zilifanyika  ukumbi wa New Msasani Club jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na watu kibao kutoka pande mbalimbali za jiji.






Picha kwa hisani ya Globalpublishers

MWANDISHI WA HABARI UINGEREZA AKUTWA AMEKUFA

Mwandishi wa zamani wa gazeti maarufu duniani la News Of The World (NOTW) Sean Hoare ambaye alivujisha kashfa iliyoliyolikumba gazeti hilo kujihusisha kunasa simu za watu mbali mbali amekutwa amekufa nyumbani kwake nchini Uingereza.

Polisi nchini imesema mwili wa Hoare ulikutwa nyumbani kwake huko Watford siku ya Jumatatu asubuhi baada ya wasiwasi kuibuka kwa kutofahamu alipo na msemaji wa polisi wa kituo cha Hertfordshire amesema kifo hicho kinachukuliwa kama hakieleweki.

Hoare alidai katika makala yake kupitia gazeti la New York Times kuwa Andy Coulson ambaye kwa sasa ni msaidizi wa waziri mkuu wa Uingereza alimshawishi kunasa mawasiliano ya simu.