.

Tuesday, July 19, 2011

JENNIFER LOPEZ NA MARC ANTHONY WAJARIBU KUNUSURU NDOA YAO



Baada ya kutangaza kutengana wanandoa Jennifer Lopez na Marc Anthony wamekenda kufanyiwa ushauri nasaha wakihaha kujaribu kunusuru ndoa yao.

Wanandoa hao ambao walitangaza kutengana siku ya Ijuma lakini watu wao wa karibu wamesema kuwa wamekuwa na msuaguano wa muda mrefu.



Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana zinasema kuwa Jennifer amejitahidi kwa uwezo wake kuifanya ndoa hiyo idumu kwa kwenda katika vituo mbalimbali vya ushauri nasaha na alikuwa mvumilivu na mwenye mapenzi na kufanya chochote alichioambiwana mumewe lakini sasa amechoshwa.

50 CENT KUSAIDIA WENYE SHIDA



Rapa 50 Cent ana nia ya kutumia nafasi yake pamoja na ushawishi alionao katika jamii kuwasaidia wenye shida na tayari ameshajiwekea lengo la kuwalisha waafrika bilioni moja.

Mkali huyo wa muziki warap ulimwenguni alibadili maisha yake kutoka uuzaji wa dawa za kulevya Jijini New York na kuwa miongoni mwa wasanii wakali wa hip hop na kupata pesa nyingi tangu mwaka 2003.


Na sasa nyota huyo wa muziki wa hip hop anataka kugawana na wenye shida kipato chake kwa kutilia mkazo ndoto yake ya kuwasaidia watu wenye njaa barani Afrika.

LADY GAGA AKABILIWA NA WAHALIFU WA MTANDAO


Nyota wa muziki nwa mwanamapinduzi wa mitindo ambaye haishiwi vituko Lady gaga amewaita polisi baada ya wahalifu wa mtandao ''maharamia'' kuishambulia tovuti yake binafsi na kuiba taarifa za mashabiki wake.

Tovuti hiyo ya Gaga imevamiwa na maharamia hao wa mtandao ambao wamechukua taarifa za siri za mashabiki zikiwemo majina yao na anuani za barua pepe zao.

Wawakilishi wa Lady Gaga wamesema wahalifu wameiba taarifa zilizokuwepo kwenye database ya tovuti zikiwemo za majina yote mawili ya baadhi ya mashabiki wa msanii huyo.

Monday, July 18, 2011

EPIQ NATION YA EATV YAWASHA MOTO...MWEMBEYANGA!!!!


Bob Juniour na mwanadada Nuru The Light wakikamua Muhongo na Andazi

Nuru the light na Rais wa Masharobaro Bob Junior wakiperfom kwenye shoo

TMK Wanaume wakifanya Shoo ndani ya Epiq Nation ya EATV


Watu Peeeeeplee!!!!

Mzee Yusuph akiwakilisha ndani ya Epiq Nation na EATV

Dancers wa Mzee Yussuph wakifanya makamuzi

Nyomi la raia wa Mwembeyanga

TMK Wanaume


Chidy Beenz Mzuka ulipanda.......

Sunday, July 17, 2011

HAPPY BIRTHDAY MWAMBA WA AFRIKA KUSINI


Afrika Kusini leo tarehe 18 July 2011 inasherehekea siku ya kuzaliwa ya rais wa zamani wa nchi hiyo Nelson Mandela ambaye anatimiza miaka 93.


Mandela anasherekea siku hiyo akiwa na afya nzuri huku taasisi yake ikiwa imetoa wito kwa kuwataka wananchi kufanya kazi za kujitolea kwa dakika 67 kwa siku hii ya leo kusherehekea miaka 67 aliyojitolea kupigania uhuru wa watu wa Afrika Kusini.

Nyota huyo ambaye ni mwamba aliyepigani uhuru wa taifa hilo na anayepingana na ubaguzi wa rangi anatarajia kutumia siku hii na familia yake katika kijiji alichokulia Mashariki mwa Cape ambapo watoto wa shule yenye watoto milioni 12.4 inatarajia kumuimbia mfululizo kumpongeza.


Tunamtakia maisha marefu zaidi yenye afya njema daima....Happy Birthday Nelson Mandela.........!!!!!!

Friday, July 15, 2011

PATTY LABELLE




Jina lake halisi ni Patricia Louise Holt Edwards alizaliwa miaka 67 iliyopita ni mwanamama mwimbaji kutoka nchini Marekani,mwandishi pamoja na mwigizaji pia.Patty Labelle alitumia miaka 16 kama mwimbaji kiongozi wa kundi la  Patti LaBelle and the Bluebelles ambalo lilibadilisha jina na kuitwa Labelle mwanzoni mwa miaka ya 70 na kutoa nyimbo maarufu ya disco ilipewa jina la "Lady Marmalade".






Mwanamama huyo aliolewa mwaka na mume wake Armstead Edwards Julai 1973 na kumzaa mtoto wao wa kwanza na wa pekee Zuri Kye Edwards na mwishoni mwa mwaka 1970 Labelle na mume wake Edwards waliasili watoto Stanley na Todd baada ya mama yao kufariki kwa ugonjwa wa saratani.




Patty Labelle ameendelea kukonga nyoyo za watu kwa vibao vyake vikali vya miaka hiyo vinavyotamba hadi leo na huchoki kusikia kwenye masikio yako kama ''If You Asked Me To'',"Stir It Up" na "New Attitude" na nyimbo nyingine kama "You Are My Friend" na "Love, Need and Want You" na ameshawahi kupata tuzo nyingi kupitia fani yake ikiwemo hivi karibuni alipopata tuzo ya Life Time Archivement Award ya BET.

JAJI MWENYE HURUMA NCHINI MAREKANI

Jaji mwenye huruma nchini Uingereza amewashangaza watu waliokuwa mahakamani baada ya kuhairisha hukumu ya  kwenda jela ya mama mmoja ili aende kwanza nyumbani kuwaaga watoto wake kabla ya kuswekwa jela.

Jaji huyo John Wait aliafiki kuwa mama huyo Sandra Hook aliyekuwa mhasibu na kuiba paundi elfu 25 za halmashauri, kuwa anapaswa kwenda kuwakumbatia watoto wake na kuwaga kabla ya kifungo.


 
                                                                   Sandra Hook
Jaji huyo wa mahakama ya Wolverhampton Crown alilazimika kuiharisha hukumu hiyo hapo jana hadi leo, ili mama huyo akawaage wanae na kuwaambia hatorudi tena nyumbani kwani anakabiliwa na kifungo jela.

LIL WAYNE ATOA ''MIXTAPE'' YA BURE

Rapa Lil Wayne amewapatia mashabiki wake watiifu mixtape ya bure  kuwashukuru kwa kuwa wavumilivu kungojea album yake mpya ambayo imekuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu.





Hali hiyo imemfanya rapa Lil Wayne kujaribu kuwapooza mashabiki wake watiifu kwa mixtape aliyoipachika jina la 'Sorry 4 The Wait'.

CHRIS BROWN AVILAUMU VYOMBO VYA HABARI




Nyota wa RnB Chris Brown amevitupia lawama vyombo vya habari kwa kutengeneza stori inayomtuhumu kuonyesha ishara ya kuwadhihaki mashoga katika mchezo wa mpira wa kikapu uliofanyika hivi karibuni.


Chris Brown akitoa shukrani katika tuzo za BET

Nyota huyo anayejaribu kujenga wasifu wake kwa jamii tangu tukio la mwaka 2009 la kumtwanga aliyekuwa mpenzi wake Rihanna, inadaiwa alishindwa kudhibiti hasira zake wakati akicheza mpira kwenye gym jijini Los Angeles na kuonyesha ishara ya kudhihaki mashoka kwa mchezaji mwingine.

Kwa mujibu wa jarida moja nchini Marekani, Brown alitoa lugha chafu na kumdhihaki mpinzani wake kwa kutembea kishoga pamoja na kumuonyesha ishara kuwadhihaki mashoga.

Thursday, July 14, 2011

''RAIS WA TAFF JIUZULU AMANI IPATIKANE''

Baadhi ya wasanii wa Filamu wa Bongo Movie Club wamemtaka rasi wa shirikisho la wasanii wa filamu TAFF Bw. Simon Mwakifyamba kujiuzuru mara moja ili amani ipatikane katika tasnia hiyo kwani wamedai yeye ndio chanzo cha mvurugano uliotokea hivi sasa unaowasabishia malumbano baina yao.

Wasanii hao Jacob Steven''JB'',Steven Kanumba,Chiki Mochoma ambaye ni mmoja wa viongozi wa klabu hiyo pamoja na mwanadada Jackline Wolper wamedai kuwa Simon ndio mchonganishi na anawachafua wao pamoja washirika wake na kusema wao klabu yao imesajiliwa na wana mamlaka ya kufanya vyovyote kwasababu haihusiani na tasnia ya filamu.

Katika sakata la Wolper kudaiwa kutaka kumpiga rais wa Shirikisho katika mkutano uliofanyika Leaders Club Wolper mwenyewe amejitetea kuwa hakuwa na nia ya kupigana bali alikuwa anataka kupishwa kwenda kumwelewesha rais alikuwa anakosea.






Tuesday, June 14, 2011

"WAHESHIMIWA MPOOOOO?"



Rais Barack Obama na swaiba wake David Cameron wakijianda kwa mazoezi ya kucheza mpira wa meza (TABLE TENNIS)
 
 
"GIVE ME GWARA"
"KUMBE NA YEYE ANATUMIA MA-LEFT KA MIMI?"
"UTAJUA KWA NINI WAZUNGU WENZAKO WAMENIPA UONGOZI WA USA"
 
 
"OOHHH KWELI WEWE MKALI KAKA"
 
 

"TUPENDE VYA KWETU ASILI YA BABU ZETU"


BHOKE ALIPOPOKELEWA NA MAMA YAKE.
 
HAPA AKIFANYA MAHOJIANO NA WAANDISHI WA HABARI.
 

 
BHOKE EGINA.
 

Monday, June 13, 2011

DOGO NAYE APATA AMPENDAYE.

JUSTIN BIEBER NA MPENZI WAKE

 







    



"Baby me naona hapa hapafai ni bora tuhame au wewe unasemaje?"
 
 
"Huku safi sana maana tuko peke yetu"
 
"Sasa tunaweza enda fanya mambo yetu ndani" Huyo ni Justine Drew Bieber(17) akiwa na mpenzi wake ajulikanae kwa jina la Selena Marie Gomez (18)

"KWEWLI JELA NJAA"

Jamaa akimlamba mkewe, sasa sijui ni njaa au ndyo malavidavi?